loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba majeruhi yaivaa Mtibwa

KOCHA wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wanahitaji ushindi ili kurudisha furaha kwa mashabiki wao kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Simba licha ya kuongoza kwa pointi 50 kwenye msimamo wa ligi hiyo, lakini kikosi hicho kinaingia kwenye mchezo wa 21 kikiwa na maumivu makali baada ya kuanza mchezo uliopita wa mzunguko wa pili kwa kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Sven amebainisha kwamba anawafahamu vizuri wapinzani wao kwani ni timu iliyosheheni wachezaji wenye ushindani na watakuwa kwenye Uwanja wa nyumbani, hivyo wanatarajia mechi itakuwa ngumu, lakini kikubwa Simba wanahitaji pointi tatu.

“Kila mmoja anajua tumetoka kupoteza, lakini tumejipanga kwa kupata matokeo mazuri kurudisha morali kwa wachezaji kuzidi kupambana na mechi zijazo lakini kuwapa furaha mashabiki wetu kwani wamekasirishwa na kilichotokea kwenye mechi tuliyopoteza juzi, ” alisema.

Wanakutana na Mtibwa inayoshika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa ni miongoni mwa timu ambazo zimekuwa kinara kwa kuzitibulia mipango timu vigogo ingawa kikosi hicho kimefanya vibaya kwenye mechi tatu mfululizo.

Kwa msimu huu hadi sasa timu hizo zimekutana mara mbili huku kila mmoja ikishinda mara moja moja, walipokutana kweye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba walishinda kwa mabao 2-1 na katika michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofanyika Zanzibar, Mtibwa walishinda kwa bao 1-0.

Kwa ujumla matokeo hayo yanaonesha wazi mchezo huo utakuwa na upinzani mkali na presha kwanza kwa Simba wanaohitaji ushindi kurudisha matumaini kwa mashabiki wao, ambao tayari wameanza kupoteza imani na timu yao, hasa baada ya kufungwa na Ruvu Shooting.

Aidha, Mtibwa hawawezi kukubali kuachia pointi kirahisi kwenye uwanja wao wa nyumbani kwani watakuwa wamejipanga kiushindani na kisaikolojia ili kujitengenezea mazingira ya kubakisha ushindi na kufuta mkosi uliowafanya kupoteza mechi tatu zilizopita.

Mechi zingine leo, Singiza na Namungo, Lipuli dhidi ya JKT Tanzania, Mwadui na Ndanda, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons, Kagera Sugar watatoana jasho na Alliance, Biashara itakumbana na Mbao, Azam na Polisi Tanzania.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi