loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga ni mwendo mdundo

KIKOSI cha Yanga leo kitaikabili timu ya Mbeya City ukiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 Usiku.

Timu hizo zinakutana mara ya 14 huku Yanga ikiwa inajivunia rekodi nzuri ya kushinda mechi 10, sare tatu na kufungwa mchezo mmoja ambao kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Mechi ya leo ni ya marudiano baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Desemba 24 na timu hizo kwenda suluhu. Timu hizo zinakutana zote zikitoka kushinda mechi zao za mwisho, Yanga ikiwa nyumbani iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0, wakati Mbeya City wakiwa ugenini Uwanja wa Jamhuri Dodoma waliwafunga ndugu zao wa Mbeya, Tanzania Prisons bao 1-0.

Yanga chini ya kocha Luc Eymael itaingia kwa nguvu katika mchezo huo ili kusaka ushindi wake wa tano mfululizo, huku ikijivunia kuimarika kwa kikosi chake kutokana na usajili walioufanya kwenye dirisha dogo ambao umeibadilisha timu hiyo kiuchezaji ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu.

Mshambuliaji David Molinga ‘Falcao’ anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya Yanga sambamba na Mapinduzi Balama, Benard Morrison na Haruna Niyonzima ambao wameonekana kuing’arisha timu hiyo, huku kocha Eymael leo akitarajia kumtumia beki mkongwe Kelvin Yondani na mshambuliaji Tariq Seif ambao wamekosekana katika mechi za hivi karibuni kutokana na majeruhi.

Yanga iliyopo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 37, inahitaji kushinda mchezo wa leo ili kupunguza gepu la pointi kati yao na Azam FC iliyopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 41 huku mashabiki wao wakitaraji kuona mabadiliko ya kiuchezaji, kwani katika mechi mbili zilizopita timu hiyo imeonekana kucheza vizuri kipindi cha kwanza ma kuishiwa pumzi kipindi cha pili.

Mbeya City iliyopo chini ya kocha Amri Said, licha ya ushindi walioupata mbele ya Tanzania Prisons, lakini haipewi nafasi ya kushinda mchezo huo kutokana na mwenendo mbaya uliooneshwa na timu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu.

Timu hiyo imeonesha mapungufu mengi ikiwemo kumtimua kocha wake Juma Mwambusi lakini pia kutumia idadi kubwa ya wachezaji chipukizi, kunaonekana kuigarimu timu hiyo ambayo ilifanya vizuri katika msimu wake wa kwanza na kujizolea umaarufu mkubwa nchini.

Kocha Amri Said atakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha anawapa mbinu mbadala wachezaji wake waweze kupambana na kuifunga Yanga ili kuendelea kujinasua katika janga la kushuka daraja, kwani timu hiyo ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo na mechi ya leo ni 21.

Said alisema kuwa timu yake imejipanga vizuri lakini anajua kuwa mchjezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Yanga na hivi karibuni imezidi kufanya vizuri katika mechi zake zote. Hatahivyo, alisema kuwa pamoja na yote watahakikisha wanalinda heshima ya Mbeya City kwa kupata matokeo mazuri katika mchezo huo, ambao utakuwa mgumu.

JUMLA ya mapambano 10 ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi