loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kurejeshwa fedha uhujumu ushindi kwa nchi

HATIMAYE Tanzania imefanikiwa kukusanya kiwango kikubwa cha fedha kutoka kwa watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi na pia kutokana na kutaifi shwa kwa mali mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu.

Wakati takribani Sh bilioni 12 zimepatikana kutokana na watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kuomba msamaha na kukubali kurejesha fedha walizohujumu, zaidi ya Sh bilioni 19 nyingine zimepatikana baada ya kutaifishwa kwa mali mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu.

Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini Biswalo Mganga alisema juzi kuwa fedha hizo za wahujumu uchumi zilipatikana baada ya watuhumiwa kuomba radhi na kurejesha kiasi hicho cha fedha walichoshitakiwa kuhujumu.

Aliyasema hayo wakati akikabidhi fedha na mali hizo Hazina. Kupitia hafla hiyo DPP pia aliutangazia umma juu ya kutaifishwa kwa mali mbalimbali yakiwemo magari, fedha taslimu, dhahabu na nyumba zilizopo maeneo mbalimbali nchini.

DPP alisema thamani ya mali na fedha walizokabidhi kwa serikali ni zenye thamani ya Sh bilioni 19 ambazo hazijajumuisha thamani ya nyumba, viwanja, boti, na mali nyingine.

Hata hivyo alisema thamani ya jumla kuu ya mali zilizotaifishwa na kukabidhiwa kwa Benki Kuu kwa ajili ya kuhifadhiwa na zile ambazo zipo tayari kwenye akaunti maalumu ni zaidi ya Sh bilioni 58.6.

Upatikanaji wa fedha na mali hizi zilizokabidhiwa kwa Hazina juzi ni ushahidi wa wazi kabisa kuwa Sheria inayohusu Makubaliano Maalumu ya Kukiri Kosa (Plea Bargaining) iliyopitishwa na Bunge Septemba mwaka jana na hatimaye kusainiwa na Rais imeleta manufaa makubwa kwa nchi yetu.

Hii inatokana na ukweli kwamba kupatikana kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha katika kipindi cha muda mfupi tangu DPP alipoanza kusimamia utekelezaji wa sheria hii, kunaonesha jinsi ambavyo siku za nyuma kama nchi, tulikuwa tunang’ang’ana na kesi kwa muda mrefu huku tukiacha mabilioni ya fedha za umma na mali zilizoibwa zikipotea siku hadi siku.

Ingawa zipo kesi za uhujumu uchumi ambazo serikali ilikuwa inashinda lakini kesi hizo zilikuwa zinachukua muda mrefu na wakati serikali inaposhinda mali hizo zilizoibwa huwa zimepotea kutokana na kufichwa au kufujwa na ndugu wa washitakiwa tofauti na sasa ambapo kupitia sheria hii mpya serikali inaokoa mabilioni ya fedha na mali.

Kwetu sisi hii ni hatua kubwa na kwa dhati kabisa tunapenda kuipongeza serikali kwa kuja na sheria hii, ambayo mbali ya kuokoa fedha na mali za umma lakini pia inawezesha washitakiwa kukiri makosa na kujutia na hivyo kujenga utamaduni mpya wa kizazi kinachotambua madhara ya kuiba mali ya umma.

Kwa namna yoyote ile hatuamini kama kuwepo kwa sheria hii kutaongeza makosa ya uhujumu uchumi kwa wahusika kujua kuwa ipo fursa ya wao kukiri na kurejesha fedha walizoiba, kwani yapo maeneo ndani ya sheria ambayo yanatoa adhabu kubwa zaidi kwa wahusika wanaokiri makosa na kurudia makosa ya awali.

TANZANIA itakuwa na ugeni mkubwa wa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi