loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ubalozi wataka alama za vidole visa kwenda China

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetangaza kuwa ofisi ya ubalozi wa China nchini imeanzisha mfumo wa kuchukua alama za vidole kwa wanaoomba visa kwenda nchini humo.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali kwenye wizara hiyo imeeleza kuwa, mfumo huo ulioanzishwa Desemba 24 mwaka jana unamlazimisha muombaji kufika kwenye ofisi za ubalozi wa China kuchukuliwa alama za vidole ikiwa ni sehemu ya kukamilisha taratibu za kuomba visa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ubalozi umeeleza kuwa utaratibu huo hautawahusu wenye umri chini ya miaka 14 na zaidi ya miaka 70.

Taarifa imeeleza kuwa waombaji wenye pasi za kusafiria za kidiplomasia au pasi za kusafiria za utumishi hawatalazimika kuzingatia mfumo huo.

Wengine ambao hawatachukuliwa alama za vidole ni wanaoomba visa kwa pasi ya awali ambayo ilihusisha kuchukuliwa alama za vidole na haijamaliza miaka mitano.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo wenye matatizo ya alama za vidole kwenye vidole vyote 10 mikononi au wenye ulemavu kwenye vidole hivyo kiasi cha kutowezekana kuchukuliwa alama za vidole hawahusika kwenye utaratibu huo.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi