loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samatta atikisa mitandaoni

MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Mbwana Samatta ndiye mwanamichezo anayeongoza kwa maarufu zaidi mitandaoni kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa utafiri ulifanywa na Nairobi Sports Digital, mshambuliaji huyo wa Aston Villa ana jumla ya wafuasi milioni 1.6 kutoka kwenye mitandao ya Facebook, Twitter huku akiwa na wengine milioni 1.4 kutoka mtandao wa picha wa Instagram.

Samatta mwenye miaka 27 alijiunga na klabu cha Ligi Kuu England, Aston Villa akitokea kwa mabingwa wa Ubelgiji, Genk.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama anashika namba mbili akiwa na jumla ya wafuasi 494,000 kwenye mitandao ya Facebook na Twitter huku akiwa na wafuasi 933,000 kwenye mtandao wa picha Instagram.

Orodha hiyo inaonesha kuwa nyota wa zamani wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi anayeichezea klabu ya Al Ittihad Alexandria ya Misri anashika nafasi ya sita kwenye utafiti huo uliochapishwa kwenye tovuti ya Nairobi Sports Digital

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi