loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kobe Bryant, bintiye wamezikwa kwa siri

MWILI wa mchezaji nguli wa nchini Marekani, Kobe Bryant na bintiye Gianna maarufu kama ‘Giggi’ wamezikwa kwa siri huko California, Ijumaa iliyopita, vyombo vya habari vimebainisha.

Inaelezwa kuwa mkewe, Vanessa Bryant na familia waliamua kufanya mazishi hayo kuwa binafsi ambayo yalihudhuriwa na ndugu na jamaa ya karibu wa familia hiyo. Kobe na Giggi walifariki kwenye ajali ya helikopta huko Calabasas, California mnamo Januari 26, 2020 pamoja na watu wengine 7 waliokuwa kwenye helkopta hiyo.

Akizungumza na chombo cha habari cha ‘Entertainment Tonight’, mmoja wa waliofanikiwa kuhudhuria tukio hilo amenukuliwa akisema; ‘‘Vanessa alitaka tukio hili kuwa la kifamilia, walitaka waomboleze kama familia kwa hali isiyohusisha umma kwa ujumla.’’

Hata hivyo, ibada maalumu ya msiba inapangwa kufanyika Februari 24, mwaka huu katika viwanja vya ‘Staples Centre’. Tarehe hiyo inaelezwa kuwa na maana kwa maisha ya wawili hao kwani mwezi wa pili unawakilisha jezi namba mbili ya Gigi huku tarehe 24 ikiwa ni namba moja ya jezi mbili za Kobe akiwa anachezea Lakers.

Ibada hiyo pia itawakumbuka watu wengine saba waliofariki kwenye ajali hiyo ikiwa ni pamoja na Alyssa Altobelli, John Altobelli, Keri Altobelli, Payton Chester, Sarah Chester, Christina Mauser na Ara Zobayan ambaye ndiye alikuwa rubani wa helkopta hiyo.

MAKAMU wa Rais Samia ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi