loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nadharia ya kujitolea katika maadili

LEO katika safu hili, tutaangalia maana ya nadharia ya kujitolea (altruism) katika lengo lile lile la kuona ni mambo gani mazuri yanatakiwa kufanywa na yapi (mabaya) yasiyotakiwi kufanywa kwa mujibu wa nadharia hii, ili hatimaye tuweze kuelewa namna nadharia hii inavyoweza kutumika kukuza maadili katika utumishi wa umma.

Kwa mujibu wa Kraut kwenye makala yake ‘Altruism’ ya mwaka 2020, nadharia ya kujitolea (altruism) ni tabia ya kufanya uamuzi au matendo yanayolenga kusaidia watu wengine na si kwa lengo la kumsaidia mtenda au mtu anayefanya jambo husika.

Kimsingi kumekuwa na mijadala mingi inayolenga kujua ama tabia ya kujitolea kwa maana ya nadharia hii ipo, au la. Wapo ambao wamekuwa wakisema tabia hii haipo miongoni mwa watu na wapo waliokuwa wanasema tabia hiyo ipo.

Kwa mujibu wa Piliavin na Charng katika makala yao “Altruism, A Review of Recent Theory and Research” ya mwaka 1990, tafiti nyingi zinaonesha kuwa matendo ya kweli ya kujitolea ili kufaidisha wengine miongoni mwa watu mbalimbali yapo na ni asili ya binadamu.

Bar-Tal katika makala hayo ya Piliavin na Charng alibainisha kuwa, wanazuoni wengi wanaosisitiza umuhimu wa nadharia ya kujitolea wanaamini kuwa, ili tendo lolote liwe na uhusiano na nadharia hii, lazima kwanza liwafaidishe wengine, lifanyike kwa hiari, lifanyike kwa kukusudia na mwisho lifanywe bila kutegemea zawadi au tuzo.

Kwa muktadha huu, ni wazi kuwa jambo muhimu na la kwanza ni lazima maamuzi au mambo yoyote yanayofanyika yalenge kuwasaidia wengine na siyo mtoa uamuzi au mtendaji wa jambo husika.

Hili ni jambo muhimu kabisa ambapo tumeshuhudia watu wengi wakilitia taifa katika matatizo kwa sababu ya maslahi binafsi kitu kinachoweza kuzuilika kabisaa kwa kuzingatia nadharia hii.

Aidha, nadharia ya kujitolea inakamilika endapo watu wanapata fursa ya kufanya mambo yenye manufaa kwa wengine kwa hiari yao na siyo kwa kulazimishwa. Hii ni muhimu kwa vile mtumishi ambaye aliyejijengea tabia ya kujitoa anaweza kujitoa nyakati zote bila kutegemea usimamizi wa karibu. Maamuzi au matendo ya kujitoa lazima yafanyike kwa kukusudia na siyo kwa kubahatisha ili kukidhi matakwa ya nadharia ya kujitoa.

Hili pia ni jambo muhimu kwa vile mtu anayefanya maamuzi au matendo mazuri kwa wengine na kwa kukusudia ana uwezekano wa kufanya hivyo kwa namna nzuri zaidi wakati wote.

Vilevile ili nadharia hii iwe imetekelezwa ni wazi kuwa mtekelezaji wa nadharia hii afanye maamuzi au matendo ya kuwasaidia wengine bila kutegemea zawadi au tuzo. Endapo mtu huyu atafanya maamuzi au matendo fulani kwa kutegemea tuzo ni wazi kuwa matendo haya, yatakuwa ni ya muda tu kwa sababu pale ambapo mtu atakosa zawadi au tuzo, basi uwezekano wa kufanya mambo mazuri kwa manufaa ya wengine unakuwa mdogo au haupo kabisa.

Kwa jumla, uzingatiaji wa nadharia hii katika utekelezaji wa majukumu, unaweza kuwasaidia watumishi wa umma kutumia nguvu zao zote kuwahudumia wengine kama lengo la msingi la uwepo wao katika utumishi wa umma na kuepukana na lengo la kujinufaisha wao binafsi.

Habari njema ni kwamba kuna uwezekano kuwa tabia ya kujitolea ikatokana na mambo yote mawili kwa maana ya makuzi na asili ya mtu mwenyewe kama ilivyobainishwa na Piliavin na Charng kwa maana hiyo hata kama mtu hana asili ya kujitoa anaweza kujengewa na kujijengea uwezo wa kufanya mambo kwa faida wengine.

Hata hivyo, kwa mujibu wa makala ya “Altruism, Incentives, and Agency Theory iliyoandikwa mwaka 1994 na Jensen, ikumbukwe kuwa pamoja na uzuri wote wa nadharia ya kujitolea bado nadharia hii haiwezi kuwa suluhisho na kila jambo katika taasisi yoyote ikiwa ni pamoja na taasisi za umma.

Schulze, Lubatkin and Dino katika makala yao “Toward a theory of agency and altruism in family firms” ya mwaka 2003 wameenda mbele zaidi kwa kubainisha kuwa nadharia ya kujitolea inaweza kabisa kutishia mafanikio ya taasisi.

Kwa mfano wenye maamuzi wanaweza kufanya mambo mengi ya kuwafaidisha watumishi wengine bila kujali kiasi cha rasilimali na hivyo kuidondosha taasisi husika kimaendeleo.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Nadharia ya kujitolea katika maadili

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi