loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwanafunzi afariki akitoa mimba

MUUGUZI aliyefukuzwa kazi kutokana na kuwa na cheti feki, anayeishi katika kijiji cha Kibengwe, Dezber Kahawa (49) anadaiwa kumtoa mimba mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kilima Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema mwanafunzi huyo, Alinda Revelian (14) alifariki dunia Februari 8 mwaka huu, baada ya kutolewa mimba.

Siku ya tukio Alinda alimuaga mama yake kuwa anakwenda kuchukua dawa kwa Dezber, ambaye kijijini kwake ni maarufu kama muuguzi, kutokana na kuwahi kufanya kazi kwenye Zahanati ya Buzi iliyopo Bukoba Vijijini.

“Alikwenda kwa muuguzi huyo, baadaye akarudi nyumbani na kusema ameshapewa dawa, lakini cha kushangaza aliendelea kuumwa na kufariki dunia,”alisema Malimi.

Alisema mwili wa Alinda, ulipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na ndipo ikabainika kuwa chanzo cha kifo chake ni kutobolewa kwa mfuko wa uzazi na kuingiziwa dawa ambazo ni sumu katika jaribio la kutoa mimba.

Kabla ya tukio hilo, majirani walishaanza kumshuku mwanafunzi huyo kuwa mjamzito kutokana na kunenepa ghafla.

Alisema muuguzi huyo ‘feki’ amekuwa akiendelea kutoa matibabu kwa kificho, bila kibali chochote na tayari anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi.

Wakati huohuo, mwanafunzi wa miaka 14, Buberwa Mberwa wa Shule ya Sekondari ya Kahororo, amefariki dunia kwa kujinyonga kwa mkanda wake wa suruali, anayoitumia kama sare ya shule.

Tukio hilo ni la Februari 9 mwaka huu katika mtaa wa Rwazi Kata Kahororo Manispaa ya Bukoba. Buberwa alikuwa akiishi kwa mama yake bila kuwepo baba yake.

Kabla ya tukio hilo, Buberwa alikuta wadogo zake wakichezea mkanda huo.

Baadaye aliwanyang’anya na kupata hasira.

Aligundulika amejinyonga kwa kutumia mkanda hupo saa 5:00 usiku katika nondo ya dirisha nyumbani kwao.

foto
Mwandishi: Diana Deus, Bukoba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi