loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mzungu wa bangi yenye jamu, siagi kizimbani kesho

RAIA wa Poland, Damian Sanikowsiki (40), kesho anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kukutwa na bangi iliyopakiwa kama asali, keki, jamu na bajia.

Pia alikutwa na kiasi kikubwa cha bangi na shamba la ekari mbili ambazo hazijavunwa. Sanikowsiki atapandishwa kizimbani na mkewe Eliwaza Pyuza (29) katika Mahakama ya Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Kamishna Jenerali wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, James Kaji alisema kuna vipimo vinavyokamilishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali na kesho watapandishwa kizimbani.

Alisema bangi iliyopo shambani ambayo bado ni mbichi wamebaini kuwa ni kilo 278, ambayo tayari ilivunwa na kukaushwa ni kilo 38.3, bangi iliyopakiwa kwa mfumo kama asali ni kilo mbili na keki ni kilo moja.

Mtuhumiwa alikamatwa mwishoni mwa wiki kufuatia operesheni maalumu iliyongozwa na Kamishna jenerali huyo.

“Tulimkamata Jumamosi na tumebaini hana kibali cha kuishi hapa nchini, anatumia ‘tourist visa’ (viza ya utalii) na amekuwa akienda uhamiaji wanamgongea kibali, kuna watu pale ambao sio waaminifu, wanacheza mchezo mchafu na mzungu huyu,” alisema Kaji.

Alisema pia katika mahojiano yao na raia huyo wa Poland wamebaini kuwa yupo nchini kwa mwaka wa tano sasa na anajishugulisha na biashara hiyo ya bangi.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamishina Jenerali, mtuhumiwa amekamatwa pamoja na mkewe, bado wanamshikilia na kwamba wanakamilisha kukusanya vielelezo na muda wowote kesho atapandishwa kizimbani.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Jumapili akiwa na bangi iliyoongezewa thamani kwa kuiweka kwenye keki na nyingine iliyosindikwa mfano wa asali, Jamu, bajia na nyingine zimekaushwa huku bidhaa hizo zikiwekewa nembo inayoonyesha zimetengenezwa nchini Australia.

“Wabunge wetu wanapigia upatu kilimo cha bangi, hawa wanaokuja nchini kwa kigezo cha wawekezaji wengine sio waaminifu, ndio kama hawa, watabeba bangi nzima,” alisema.

Kwa mujibu wa mtuhumiwa huyo ni kwamba bidhaa zake hutumiwa na wateja wa ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka yote mitano alichokua nchini.

“Vyombo vya ulinzi na usalama kuanzia ngazi ya kijiji, vipo mtu analima bangi kwa miaka yote hiyo bila kujulikana, aliona serikali imelala, sasa ipo macho, tutaendeleza na operesheni hii na mikoa mingine,”alisema

MFUMO wa kielektroniki wa ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi