loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Askofu: Utalii wa asili chachu ya maendeleo Upareni

Utalii wa asili umekuwa chachu ya kufungua maeneo mengi yaliyokuwa hayajulikani kabisa kama vivutio vya utalii, Upareni, na kwingineko.

Maneno hayo yalisemwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Pare, Dk Charles Mjema hivi karibuni, kwenye hafla maalum ya kumpa daraja la uchungaji Mama Witness Issa.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na wageni kutoka Ufaransa, Ubelgiji na Marekani, Askofu alimshukuru sana mratibu wa shughuli za utalii Same Elly Kimbwereza, kwa kusimamia utalli wa asili kuleta maendeleo Upareni.

Kimbwereza kupitia Utalli wa Asili amesimamia ukarabati majengo na barabara katika zahanati ya Mbaga, Manka iliyojengwa tangu enzi za utawala wa Wajerumani katika vilele vya milima ya Pare Kusini eneo la Mbaga.

Aidha amekuwa akielimisha watu wa eneo la Mbaga ambalo limesheheni majengo mengi yaliyojengwa enzi za wajerumani zaidi ya miaka 120 iliyopita kuona umuhimu wa majengo hayo katika utalii wa asili.

Majengo hayo ni pamoja na zahanati, nyumba za kuishi watumishi na kanisa lililojengwa wakati mmoja na kanisa la Azania Front liloloko jijini Dar es salaam.

Majengo hayo bado yanatumiwa kwa kadri ya shughuli zilizonuiwa mwanzo. Majengo hayo yote yanamilikiwa na KKKT Dayosisi ya Pare. Naye Elly Kimbwereza pamoja na kumshukuru askofu huyo kwa ushirikiano anaopata toka viongozi wa dini katika kufanikisha utalii wa asili, ameitaka jamii kuendelea kuwajibika kufanikijsha utalii huo.

Aliwaomba viongozi wa dini walioalikwa kanisani hapo katika hafla ya chakula cha mchana kutumia nafasi zao kuwakumbusha wenzao wa barani Ulaya wajibu wao sio wa kiroho tu bali na kuhakikisha wanaiendeleza jamii kiuchumi kwa kutangaza waliyoyaona wakati wakiwa nchini.

Kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha utalii asili na jinsi anavyofahamu historia ya maeneo hayo ya Mbaga, Elly Kimbwereza aliwahi kwenda Ujerumani kuwakilisha kanisa kwenye shughuli maalum ya kamati ya Fungamano La Makanisa ya Kilutheri Ujerumani iliyoandaa sherehe ya miaka 500 tangu kuasisiwa kwa kanisa hilo.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Same

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi