loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wadau mafunzo utalii watakiwa kuunganisha nguvu kuinua tija

SERIKALI imezitaka taasisi za mafunzo na wadau wa sekta ya utalii kuunganisha nguvu ili kutatua changamoto zilizopo, ikiwemo nguvu kazi yenye weledi katika tasnia hiyo.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha wakati akifungua kongamano la kimataifa la kuunganisha wanataaluma na wadau wa sekta ya utalii na ukarimu.

Alisema katika mazingira ya sasa ya ushindani kunahitajika maandalizi mazuri ya rasilimali watu ili kuweza kushindana. Alisema utalii ni moja ya sekta inayolipatia taifa fedha za kigeni akitolea mfano mwaka jana nchi ilipata fedha za kigeni dola za Marekani milioni 2.4 kutokana na utalii, hivyo kukiwa na nguvu kazi yenye weledi na ufanisi wa kutosha nchi itaneemeka kupitia utalii.

Naye Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dk Shogo Mlozi alisema kwa kushirikiana na vyuo vingine vinavyotoa mafunzo ya utalii, wataendelea kuimarisha mpango wa utoaji mafunzo kwa kufanya kazi karibu na watoa huduma ili kupata nguvu kazi yenye weledi na ujuzi.

Kwa upande wake mshiriki wa kongamano hilo kutoka VETA makao makuu, Happiness Salema alisema ni vizuri kukawa na makongamano ya aina hiyo kwa kuwa yanawaleta pamoja watoa mafunzo na wamiliki wa viwanda, jambo ambalo linasaidia kuona changamoto zilizopo na kuweka mkakati kwani nchi zilizoendelea zinatumia mfumo

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments