loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa azindua Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maagizo kumi wakati akizindua Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma, ambao utekelezaji wake katika miradi iliyopo na ijayo, utagharimu takribani Sh trilioni 4.1.

Akizindua Mpango huo jijini hapa jana, Waziri Mkuu alisema Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Tamisemi, wanatakiwa kutekeleza Mpango Kabambe kama unavyoelekeza kwa maendeleo ya jiji na makao makuu ya serikali.

Waziri Mkuu alisema Jiji la Dodoma, linatakiwa kupima viwanja kwa kasi kubwa zaidi ili kwenda na kasi ya ongezeko la watu, kwani kasi ndogo itachangia kupata ujenzi holela.

Alisema Jiji la Dodoma wanatakiwa kufanya mapitio ili kasi ya upimaji wa viwanja, itanguliwe na ufikishaji wa miundombinu mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo maji, umeme, barabara na huduma nyingine na uboreshaji wa mitaa na uwekeji taa barabarani.

Waziri Mkuu alisema Mkurugenzi wa Jiji, anatakiwa kufuatulia kwa karibu na kufanya tathmini ya ujenzi wa jiji kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Namba 14 (3) ya mwaka 2007 ili kwenda sambamba ili kupata makazi bora na kuhakikisha changamoto zinatekelezwa.

Alisema Jiji la Dodoma linatakiwa kutangaza fursa za viwanja katika mitandao mbalimbali, kwa kutumia pia vyombo vya habari na taasisi nyingine ili kupata huduma hizo jijini hapo.

Alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuongeza kasi ya kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali kwa kuwa kumekuwa na malalamiko ya kutozwa nguzo kwa wakazi wa maeneo ya Makulu, Mkalama, Nala na mengineyo kwamba tangu mwaka jana Desemba wamelipa, lakini umeme bado.

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments