loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bashe aunda kamati ya watu 12 kuinua zao la zabibu

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameunda kamati ya watu 12 itakayoandaa ripoti ya namna ya kukuza zao la zabibu. Alisema zao la zabibu ndio uti wa mgongo wa Jiji la Dodoma, hivyo kuna kila sababu ya kuwa na mpango mkakati kwa ajili ya kuinua zao hilo.

Bashe alisema hayo juzi wakati wa mkutano na wadau wa zao la zabibu waliokuwa wakijadili changamoto mbalimbali zinazokabili zao hilo. Bashe alisema, zabibu Dodoma inazalishwa kwa kudra za Mwenyezi Mungu, ndio maana ameamua kuunda, Timu ya Kitaalamu (technical team) ili iweze kuleta ripoti itakayofanyiwa kazi.

Kamati hiyo ya watu 12 itakaongozwa na Mwenyekiti, Gungu Mibavu kutoka ofisi ya Sera, Mipango na Maendeleo (DPP) ya wizara hiyo, ambapo wote watafanya utafiti kwa muda wa wiki moja na kuwasilisha ripoti.

“Ripoti itakayoletwa na kamati hii, itatusaidia kujua wakulima wa zabibu wako wangapi? Changamoto za wakulima, wazalishaji na wasindikaji, hivyo itatusaidia katika mikakati yetu,” alisema Bashe.

Aidha Bashe alisema, mkakati mwingine wa serikali ni kufufua mabwawa yote yaliyotengenezwa kwa ajili ya umwagiliaji wa zabibu katika wilaya tatu zinazolima zao hilo ambazo ni Bahi, Chamwino na Dodoma. Bashe amewataka wadau wa kilimo cha zabibu kuunda vyama vya ushirika ili viweze kusaidiwa kwa karibu na taasisi za fedha.

Naye Mkurugenzi wa Doniya Estate ambaye ni msindikaji wa zao la zabibu, Catherine Mwambie alisema kuwa suala la tozo limekuwa kikwazo kikubwa kwa wazalishaji wa mvinyo.

“Yaani kwa siku moja zinakuja taasisi zaidi ya tano, kila moja inakuja kuchukua kodi, sasa tunajikuta hata faida hatupati, maana hela yote inaishia kwenye hizo kodi,” alisema Mwambie.

Aidha Mwambe alisema gharama za uzalishaji ziko juu, na soko la zabibu hapa nchini bado, hivyo waniomba serikali kuingilia kati, kuweka mazingira rafiki ya biashara ya zabibu.

Msindikaji mwingine wa zabibu, Sylivester Wambura alisema, changamoto ni kuuziwa zabibu kwa bei kubwa kutokana na wakulima wanavyotumia gharama kubwa kwenye uandaaji hadi mavuno ya zabibu.

“Mvinyo wa zabibu ambao unapatikana Dodoma huuz- wa kwa gharama kubwa kuliko mvinyo unaotoka nje ya nchi kutokana na gharama za uzalishaji,” alisema.

Alisema anamfahamu mtaalamu mmoja tu wa zabibu lakini kama kutakuwa na wataalamu wengi wa kusaidia wakulima kwa ajili ya kulima, kukatia matawi mpaka namna ya kupulizia dawa zao la zabibu ambayo inapatikana Tanzania pekee inaweza kushuka na zabibu ya Tanzania ikawa bora zaidi.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi