loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tarura yahitaji mil 700/- kurejesha miundombinu

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mkoa wa Dodoma imepeleka maombi serikalini ya Sh milioni 700 kwa ajili ya kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja mkoani humo.

Kauli hiyo aliitoa Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dodoma, Lusako Kilembe katika Mkutano ulioitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene.

Kilembe alisema kutokana na uharibifu wa miundombinu mingi katika wilaya zote saba za mkoa huo, wakala huo umefanya tathmini na kubaini kwamba wanahitaji fedha hizo ili kurejesha miundombinu hiyo mara mvua itakapokoma.

“Marekebisho hayo yatahusisha uboreshaji wa barabara na madaraja katika maeneo mbalimbali mkoani humo ili zipitike tena,” alisema.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Simbachawene baada ya kusikiliza mkakati huo, aliwataka Tarura kuhakikisha barabara na madaraja yaliyosombwa katika jimbo lake la Kibakwe na katika wilaya ya Mpwapwa kwa ujumla yanarekebishwa ili kurejesha huduma ya usafiri katika maeneo mbalimbali jimboni humo.

Aliwaomba wananchi wa maeneo mbalimbali jimboni humo, waendelee na kilimo cha mazao yanayohitaji mvua kidogo kama njugu na karanga, wakati serikali ikishughulikia kurekebisha miundombinu iliyoharibika, badala ya kukaa kwenye mitandao kulalamikia ubovu wa barabara.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alisema wilaya hiyo imepata changamoto ya barabara nyingi pamoja na madaraja kuharibika hivyo ili kupitika yanahitaji kurekebishwa ili kurudi katika hali yake ya awali. Awali kabla ya mvua kuharibu mtandao wa barabara zilihitajika jumla ya Sh milioni 12,635.16 kwa ajili ya kugharamia kazi za matengenezo ya barabara mkoani.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Mpwapwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi