loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Eymael, Manara wapelekwa Maadili

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewapeleka kwenye Kamati ya Nidhamu na Maadili makocha na wasemaji wa timu za Simba na Yanga.

Makocha hao pamoja na wasemaji wamepelekwa kwenye kamati hiyo baada ya kushutumu na kutoa matamshi yenye kukashifu na kudhalilisha viongozi, chapa ya ligi na taasisi kwa ujumla kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa vipindi tofauti.

Hayo yalibainishwa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo jana. Ndimbo alisema katika kikao cha Februari 10, Kamati ya Uendeshaji ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi mbalimbali.

Alisema wanaopelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu na maadili kujibu tuhuma zao ni kocha wa Yanga, Luc Eymael, msemaji wa Simba, Haji Manara na mhamasishaji wa Yanga, Anthonio Nugaz pamoja na kocha wa Namungo FC, Thierry Hitimana.

Alisema kocha wa Simba, Sve Vandenbroeck ametozwa faini ya Sh 500,000 kwa kugoma kuongea na waandishi baada ya mchezo kumalizika na amepewa onyo kwa kosa la kugoma kuwafungulia mlango mwamuzi na kamishina wa mchezo wakati wa ukaguzi wa timu katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Februari 1, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Klabu ya Polisi Tanzania imepigwa faini ya Sh 1, 500,000 kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi wa kuingia uwanjani katika mechi iliyochezwa Februari 4, katika Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na adhabu hii ilitolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(14).

Mchezaji wa Azam, Agrrey Moris amepigwa faini ya kiasi cha Sh 200,000 kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi iliyochezwa Februari 5, katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Pia kamati hiyo imewafungia waamuzi watatu miezi mitatu kila mmoja kwa makosa ya kushindwa kutafsiri sheria na mwingine kumudu mchezo.

Mwamuzi Abubakar Mturo ambaye alichezesha mchezo kati ya Yanga na Lipuli FC naye amefungiwa kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo. Mwamuzi msaidizi namba mbili, Joseph Pombe amefungiwa kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo na mwamuzi msaidizi namba mbili, Kassim Mpanga kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu.

JUMLA ya mapambano 10 ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi