loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Twiga Stars karata muhimu leo

TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, inatarajia kuvaana na timu ya Mauritania katika mechi ya kwanza ya kuwania ubingwa wa mashindano ya UNAF itakayochezwa kwenye Uwanja wa Kram ulioko nchini Tunisia, leo.

Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 11:00 kwa saa za Tunisia sawa na saa 7:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki katika mashindano hayo yanayoshirikisha nchi tano.

Akizungumza akiwa nchini humo jana, Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime alisema wachezaji wote wako salama na wako tayari kuanza kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Shime alisema amewaandaa wachezaji wake kupambana na kuwa watulivu katika mchezo huo ili kuanza vema michuano hiyo na kufikia malengo ya kurejea na ubingwa. Alisema anaamini kasi waliyokuwa nayo katika mashindano yaliyopita wataiendeleza na kuiwakilisha vema Tanzania.

“Kiufundi tuko vizuri na tunaamini tutafanya vema katika mashindano haya, siwajui vizuri wapinzani wetu Mauritania, lakini baada ya kuwaona uwanjani kwa dakika 10 nitajua mbinu zaidi za kuwamiliki,” alisema Shime.

Nahodha msaidizi wa Twiga Stars, Amina Ally alisema kikosi chao kiko imara na wako Tunisia kwa kazi moja ya kusaka ushindi katika kila mechi watakayocheza. Amina alisema wanaamini wana uwezo wa kuibuka mabingwa na kulinda heshima waliyopewa ya kualikuwa kwenye michuano hii.

“Kama ambavyo wametuamini, sisi tutapambana kuhakikisha tunaanza vizuri na kujiweka katika nafasi nzuri, ukishinda mechi ya kwanza unapata nguvu ya mechi inayofuata, kila mechi kwetu ni fainali,” alisema Amina.

Mechi nyingine itakayochezwa leo itakuwa ni kati ya wenyeji Tunisia dhidi ya Morocco itakayoanza saa 10:15 jioni kwa saa za Tanzania.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi