loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kondomu bado inadhibiti maambukizi ya magonjwa

IMEELEZWA kuwa kondomu bado zinabakia kuwa njia madhubuti ya kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngono na mimba zisizopangiliwa nchini ka takriban asilimia 98.

Aidha wanawake wana fursa kubwa ya kuhamasisha matumizi ya kondomu, lengo likiwa ni kuzuia mimba zisizopangwa na hata kulinda afya kwa ujumla. Hayo yamesemwa leo jijini Dra es Salaam na Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kijamii, Kutoka shirika la T-MARC Tanzania, Flavian Ngole na kuongeza kuwa ni muhimu kwa kondomu kutumika kwa usahihi ili kujilinda.

Ngole amesema hayo ikiwa ni maadhimisho ya kimataifa ya kukuza uelewa juu ya kondomu pamoja na kuelimisha jamii umuhimu wa kufanya ngono salama muda wote na kuondoa dhana ya woga wakati wa kwenda dukani kwa ajili ya kununua kondomu.

“Maadhimisho haya yanatumika kwa ajili ya kupinga unyanyapaa ambao unahatarisha maisha ya watu wengi hususani vijana na wanawake ambao wapo kwenye hatari kubwa alisema na kuongeza kuwa watu wanatakiwa kufanya maamuzi yao wenyewe na ridhaa zao na kujifunza namna ya kutumia kondomu kwa usahihi.

Amesema Shirika hilo limekuwa likitumia njia za kibunifu kuwafikia watanzania hususani wale ambao wahajafikiwa na huduma muhimu kupitia njia zautolewaji wa huduma na bidhaa za kijamii na mawasiliano.

Ngole amesema katika kusaidia juhudi za serikali kwenye kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi, mimba zisizopangiliwa na magonjwa ya ngono, kupitia utoaji wa huduma na bidhaa kwa ajili ya kuhamasisha ununuzi na matumizi juu ya aina mbalimbali za kondomu na zenye sifa tofauti ili kuwapa watu fursa ya kuchagua.

Aidha amesema matumizi ya kifaa hicho yanatakiwa kutumika kwa makundi yote,ikiwemo walemavu lengolikiw ani kuwalinda wenza wao katika kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Aidha amesema lipo kundi kubwa la watu ambao bado hawajui kuwa wanaweza kupata kondomu bure katika klimiki za maneo yao,vituo vya afya na katika taasisi nyingine, huku wakiendelea kuona aibu kwenda madukani kununua.

Kuhusu mwanamke kuwa chachu ya matumizi ya kondomu,Meneja Utawala na Logistiki, Geraldine Duwe alisema ipo haja ya kuondolewa taswira katika jamii kuwa kununua kondomu ni tabia za uhuni jambo ambalo litasaidia kuelimishana na kuongeza uelewa juu ya matumizi yaliyo sahihi.

Amesema kwa mwanamke anayo fursa kubwa kwa matumizi hayo, na kuhakikisha kuwa kila anapokuwa na ridhaa ni muhimu kutumia kwa usahihi ili kujikinga pamoja nakulinda afya yake kwa ujumla.

“Watu wawe na uelewa sahihi wa matumizi ya kondomu, ipo haja ya kuhamasisha juu ya mahusiano mazuri na salama na kuwakumbusha watu juu ya hatari ya magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono na mimba zisizopangiliwa,” alisema Geraldine na kuongeza kuwa kila mmoja alinde usalama wake

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments