loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

REPOA yang'ara kiutafiti Africa

TAASISI inayoshughulika na masuala ya Utafiti(Repoa), imeng'ara kwa kushika nafasi ya 11 kati ya taasisi 612 zinazifanya kazi hiyo barani Afrika.

Repoa imeendelea kushikiria nafasi hiyo ya juu kwa miaka sita mfululizo kwa tanzania na kuzipita taasisi nyingine zinazofanya shughuli hizo.

Ripoti hiyo ilitolewa mwishoni mwa January mwaka huu Washington DC nchini Marekani na taasisi ya Kitafiti ya Kimataifa ya Global Think Tanks(TTCSP).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Dk.Donald Mmari, amesema taasisi yao imefanikiwa kushikilia nafasi hiyo ya 11 tangu mwaka 2017, kati ya taasisi hizo 612 Barani Afrika.

"Mafanikio haya katika taasisi yetu yametokana na kuaminiwa na kutumika kwa kazi ambazo tumekuwa tukizifanya na kuleta manufaa katika taifa letu," amesema Dk.Mmari na kuongeza: "Tunaishukuru sana serikali yetu kwa kutuamini na kwa kuona kwamba kazi zetu ni bora za kuaminika na kuendelea kuzitumia kwa kuona umuhimu wake," amesema Dk.Mmari.

Pia amesema kwamba mpango kazi mpya wa miaka mitano ijayo wamepanga kuboresha zaidi kazi zao hususani kwa kutilia mkazo katika mambo makuu matatu.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni katika ukuaji wa uchumi, katika maendeleo ya jamii na matakwa ya kidunia katika kutekeleza malengo endelevu(STGs).

Eneo jingine watakaloliangalia ni jinsia na maendeleo ya binadamu hususani katika afya na mifuko mbalimbali ya kusaidia jamii. "Tunaangalia kwa kina na namna ya kutoa ushauri wa kisera ili tofauti za kijinsia zisiwe kikwazo kwa kukua kwa maendeleo," amesema Dk. Mmari.

Eneo la tatu amesema wataangalia utawala, uwajibikaji, na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za kiuchumi. Mwisho

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments