loader
Picha

Rais Kiir apendekeza majimbo 10

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir (pichani) amependekeza kuwapo majimbo 10 badala ya 32 ya sasa likiwamo lenye migogoro la Abyei.

Chanzo kimoja cha habari kilichoshiriki mkutano wa mashauriano kuhusiana na idadi ya majimbo nchini humo kimeeleza kuwa, wajumbe wamekubaliana kuondolewa kwa majimbo tisa na kuanzisha 24, likiwamo la Abyei.

Chanzo hicho cha habari kilieleza kuwa, Rais Kiir alipendekeza majimbo ya kuondolewa kuwa ni Southern Liech, Akobo, Terekeka, Amadi, Maiwut, Tombura, Lol, Twic na Gok. Alitaja majimbo yanakayobaki kuwa ni Bieh, Fangak, Jongle, Boma, Liech, Central Upper, Fashoda, Latjor, Northern Upper Nile, Ruweng, Eastern Lakes, Western Lakes, Aweil East, Aweil, Gogrial, Tonj, Wau, Raja, Jubek, Yei,Torit, Kapoeta, Yambio, Maridi na eneo la utawala la Abyei .

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kukubali pendekezo la Muungano wa Maendeleo Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika (IGAD) la idadi ya majimbo kupungua kutoka 32 mpaka 10 au 23.

Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Michael Makuei Lueth, katika taarifa yake juzi, alisema serikali ipo tayari kutekeleza mapendekezo ya Baraza la Mawaziri la IGAD.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: JUBA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi