loader
Picha

Wananchi wavuna bil 78/- GGM

WAFANYABIASHARA wazawa wamenufaika na Sh bilioni 78 kati ya Sh bilioni 335 zilizotokana na kufanya biashara ya kutoa huduma kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa mwaka jana.

Hata hivyo, kiasi hicho bado ni kidogo kulingana na uhitaji na hivyo kwa kuliona hilo, Serikali ya Mkoa wa Geita imeingia makubaliano na mgodi huo kuhakikisha fursa ya kipaumbele kwa wazawa wenye sifa zinazingatiwa kuwapatia fursa ya kutoa huduma katika mgodi huo kuliko ilivyo sasa.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel jana wakati wa mkutano wake na wanahabari akitoa tathmini na mrejesho wa kikao cha Baraza la Biashara Mkoa kilichofanyika Februari 14, mwaka huu.

Ili kuhakikisha sheria ya mabadiliko ya manunuzi ya “Local Content 2018” ambayo inamtaka mwekezaji/ kampuni kutoa ajira, kununua bidhaa au huduma uhimlishaji teknolojia na mafunzo kwa wazawa kupitia marekebisho hayo kumekuwepo na mjadala baina ya Serikali ya Mkoa, TCCIA na GGM.

Pia imebainishwa kuwa kampuni 139 ndizo zinazofanya kazi ya kutoa huduma GGM ambazo kampuni nyingine 120 tayari zimewasilisha maombi kwa mgodi huo ili kutoa huduma kati ya 259 ya wazawa zilizoomba kufanya kazi ya utoaji huduma huku uwazi ukitakiwa ikiwemo kupitia TCCIA kuweka wazi kwa orodha ya kampuni ambazo tayari zinafanya biashara na GGM na zilizopo.

Mkuu wa mkoa ameongeza ili kuwezesha kuondoa malalamiko ya kutopata fursa tayari kumeundwa kamati itakayoshirikisha Serikali Kuu, Halmashauri, TCCIA na GGM ili kuhakikisha maazimio ya kikao cha Februari 14, mwaka huu cha Baraza la Biashara Mkoa yaliyoazimiwa yanatekelezwa.

Alisema lengo ni kuhakikisha huduma zote ambazo zinaweza kutolewa na wazawa na kwa huduma ambazo zinapatikana na katika mazingira ya jamii inayozunguka mgodi zinapewa kipaumbele na fursa kwa walengwa ili kunufaika kuliko ilivyo sasa na zinazohitaji sifa zaidi mkakati unafanyika na kwa taasisi za fedha na baadhi zimeridhia kuwashika mikono watakaofanikiwa kupata kazi ya utoaji huduma katika GGM.

Akizungumzia hatua hiyo baada ya mkutano wa wanahabari na mkuu mkoa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Leonard Bugomola alisema hatua hiyo itaongeza ufanisi na tija kutokana na kampuni nyingi baadhi zinazopewa kazi ya kutoa huduma GGM yenye makao yake yake makuu nje ya Geita kutolipa ushuru wa huduma.

“Hatua hii itaondoa usumbufu kwa makampuni yanayotoa huduma kwa mgodi wa GGM yenye makao yake makuu nje ya Mkoa wa Geita kukwepa kulipa ushuru wa huduma yaani service levy,” alisema Bugomola.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka mikoa 12 ifi kapo Septemba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi