loader
Picha

Bashe- Benki wekezeni kwenye alizeti

SERIKALI imezitaka taasisi za kifedha zikiwemo mabenki, kuwekeza katika sekta ya kilimo, hususani katika zao la kimkakati la alizeti.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe katika mkutano uliozikutanisha benki mbalimbali, wadau wa kilimo na kampuni za bima.

“Nchi inaingia gharama kubwa kununua pembejeo nje, ifike mahali tuzalishe mbegu zetu, lazima tuje na mikakati imara wakati mkulima anaenda shambani mbegu ziwe sokoni kwa gharama nafuu, ifike mahali mkulima akopesheke,” amesema Bashe.

Alisema mkakati wa serikali ni kuongeza uzalishaji wa mbegu, ambapo serikali katika mwaka wa fedha 2019/20 ilitenga takribani Sh bilioni 13 kwa ajili ya utafiti wa mbegu kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mbegu (TARI) na uzalishaji wa mbegu kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA).

Hata hivyo, akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mabenki (TBA), John Machunda ambaye pia ni Meneja Mwandamizi Biashara na Kilimo wa NMB, alisema mabenki yapo tayari kuwekeza kwa kutoa mitaji, lakini sera iliyopo ndio changamoto kubwa, kwani haitoi mwanya kwa wakulima hususani wa zao la alizeti kukopesheka.

Alisema hakuna bodi inayosimamia alizeti, kama ilivyo kwenye pamba, korosho na sukari na hivyo kufanya wakulima wa zao hilo kushindwa kukopesheka hususani wanaohitaji mikopo mikubwa.

Alitaka suala hilo lisiachiwe taasisi za mabenki peke yake na badala yake Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), nayo iingize mitaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine alisema mbegu ni eneo lenye changamoto kubwa, kwani asilimia 90 ya wakulima hawatumii mbegu bora, hivyo ni jukumu la serikali kutoa elimu kwa wakulima.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka mikoa 12 ifi kapo Septemba ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi