loader
Picha

Azam kuharibu rekodi ya Ndanda leo?

LIGI Kuu Tanzania bara inatarajia kuendelea tena leo, Jumatano, ambapo viwanja vitatu vitawaka moto kukamilisha mzunguko wa 23 wa mbio za kuwania taji hilo ambazo hadi sasa Simba ndiyo kinara wake.

Azam FC watakuwa wageni wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Nangwanda Sijao wakati Mtibwa Sugar wakiwa wageni wa Tanzania Prison mkoani Mbeya huku Alliance FC wakisafiri hadi Shinyanga kuwakabili wachimba madini wa Mwadui.

Ndada FC wanaingia katika vita hiyo leo huku wakiwa na jumla ya pointi 13 kibindoni ambazo ni pointi nyingi zaidi kuliko timu yoyote ile kwenye michezo mitano iliyopita huku wapinzani wao, Azam FC wakiwa wamefanikiwa kukusanya point nane pekee katika michezo iliyocheza hivi karibuni.

Kocha wa Azam FC, Mromania Aristica Cioaba amejinasibu kuwa ataishikisha adabu timu hiyo kwa kuvunja rekodi bora kabisa kwa ‘Wanakuchele’ ambao hawajapoteza mechi hata moja kati ya tano za hivi karibuni.

“Mchezo hauangaliwi rekodi ya nyuma, atakayecheza vizuri mara nyingi ndiye anayepata matokeo mazuri kwenye soka.

Tunajua Ndanda ina imarika kila kukicha ila tutapambana,” amesema kocha huyo Azam inaingia uwanjani kuhu wapinzani wake Yanga wakiwa wameshikiliwa shati kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kukamatwa shati na Polisi kwa sare ya 1-1 huku Simba ikijitutumua kwa kuitandika Kagera Sugar 1-0, jijini Dar es Salaam.

MSAJILI Msaidizi wa Vyama vya Michezo Jiji la Arusha, Benson ...

foto
Mwandishi: Bosha Nyanje

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi