loader
Picha

Klopp aitisha Atletico

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema atafanya kila anachoweza kuhakikisha Atletico Madrid wanapoteza mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) katika dimba la Anfield mapema mwezi ujao.

Klopp ametoa kauli hiyo baada ya kupoteza kwa goli 1-0 kwa Atletico usiku wa kuamkia leo, Jumatano, katika uwanja wa Wanda Metropolitano.

“Kilichotokea kila mmoja amekiona, sina matatizo na matokeo tulifanikiwa kuwaweka wapinzani wetu kwenye wakati ngumu ndani ya dakika 30 za mwanzo lakini hatukuwa makini kwenye kutumia nafasi tulizopata, changamoto kubwa ilikuwa kubaki mchezoni tulipoteza pia muelekeo katika ya mchezo lakini niseme wazi kuwa kazi bado haijaisha tutahakikisha wanaona maana halisi ya Anfield kwenye mchezo ujao,” alimaliza Kloop.

Aidha Kloop amesema kuwa alilazimika kumtoa mshambuliaji wake Sadio Mane kwenye mchezo huo akihofia pengine angeweza kupata kadi nyekundu na kuukosa mchezo ujao kutokana na aina ya mchezo ulionyoeshwa na wapinzani wake.

Mchezo baina ya Atletico Madrid dhidi ya mabingwa hao watetezi wa UEFA utachezwa Machi 11, mwaka huu huku Liverpool ikihitaji ushindi wa zaidi ya magoli mawili huku ikihakikisha kuwa hairuhusu goli la ugenini.

LIGI Kuu ya Ubelgiji imekuwa ligi la kwanza barani Ulaya ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi