loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yaingia hofu

KOCHA Msaidizi wa Timu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa matumaini ya timu yake kutwaa ubingwa yameanza kufi fi a baada ya juzi kulazimishwa sare kwa kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Hiyo ni sare ya tatu mfululizi kwa Yanga baada ya awali kulazimishwa sare na wababe wawili wa Mbeya, Mbeya City na Tanzania Prisons. Mkwasa alikiri kuwa matokeo hayo yamezidi kuiweka pabaya Yanga katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara huku akisisitiza kuendelea kupambana na wanajiandaa kuifuata Coastal Union na kuahidi kurekebisha pungufu. Yanga itacheza na Coastal Union Jumapili kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

“Mechi ilikuwa ngumu ingawa mchezo ulionekana uko kwetu zaidi lakini uzembe uliofanyika kuokoa mpira wa kona, ndio ulisababisha Polisi wakasawazisha lakini kulikuwa na kila dalili ya sisi kushinda, tulijipanga vizuri, “alisema Mkwasa.

Alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kucheza na timu ambayo mnakuwa mmejaribu kuweka mipango ila yenyewe inacheza kwa kupiga mipira mbele na kusema pamoja na hayo matokeo wameyakubali.

“Hatukuzidiwa sana bali ni makosa tu tumefungwa kutokana na uzembe katika nafasi ya ulinzi ila kiujumla kipindi cha pili hakikuwa kizuri sana sababu wao walipata goli na sisi tulikuwa na wachezaji ambao waliumia, “alisema Mkwasa.

Naye muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema wameyapokea matokeo na kutoa angalizo kuwa ligi ni ngumu.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Moshi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi