loader
Picha

Maxime aukubali muziki wa Simba

KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kwa kiwango kilichooneshwa na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu juzi hakikuwa cha kawaida, hivyo kufungwa kwao, walistahili tena kwa mabao mengi.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wekundu hao walishinda bao 1-0, kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Meddie Kagere.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo juzi, Maxime alisema walishambuliwa sana na wapinzani wao kiasi kwamba kama wangekuwa wametulia wangeadhibiwa kwa idadi kubwa ya mabao huku akikiri mpira una matokeo yasiyotarajiwa.

“Niwapongeze Simba kwa mchezo wa leo (juzi), tulishindwa kumiliki mpira tukawapa nafasi ya kutushambulia, lakini pia, niwapongeze wachezaji wangu kama sio umakini pengine tungekuwa tumefungwa mabao mengi zaidi,”alisema.

Maxime aliwapa pole wachezaji wake akisema walicheza kwa kiwango cha chini tofauti na walivyozoeleka. Alisema wanajipanga katika michezo ijayo wasirudie makosa yaliyojitokeza. Kwa upande wa Kocha wa Simba, Sven Vandebroeck aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kiwango bora akihimiza kuendeleza moto huo katika michezo ijayo.

Alisema walistahili kushinda, kwani walimiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi ila ni kama walijiadhibu kwa sababu walipata ushindi finyu wa bao 1-0 ndani ya dakika 90.

“Wachezaji wangu walionesha uwezo kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo kama wangezitumia vizuri wangefunga mabao mengi, lakini tunapaswa kujilaumu kutokana na kushindwa kutumia nafasi kadhaa tulizotengeneza,”alisema.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi