loader
Picha

Wahariri HabariLeo waula TFF

WAHARIRI wa gazeti hili ni miongoni mwa wadau wa michezo walioteuliwa tena na Kamati ya Utendaji ya Shiriksho la Soka Tanzania (TFF) kuunda Kamati ya Maendeleo na Miradi, imeelezwa.

Mhariri wa habari, Mgaya Kingoba na Mhariri wa Michezo wa gazeti hili, Zena Chande walitajwa jana kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kamati hiyo, baada ya kufanywa kwa mabadiliko katika kamati mbalimbali.

Kingoba na Zena wameteuliwa tena katika kamati zao baada ya kuwa wajumbe katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, huku Kingoba akiwa mjumbe pekee aliyerudi katika Kamati ya Habari na Masoko.

Kamati ya Habari na Masoko inaongozwa na Steven Mnguto (Mwenyekiti), Osuri Kosuri, Cyprian Kuyava, Mgaya Kingoba, Dk Omar Saleh na Saleh Ally. Zena ni mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, ambayo inaongozwa na Amina Karuma (Mwenyekiti), Mia Mjengwa (Makamu Mwenyekiti), Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma na Zabibu Juma.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka TFF, Kamati ya Utendaji ilikutana juzi na kufanya mabadiliko na kupokea taarifa ya maandalizi ya utekelezaji wa miradi kwenye kikao kilichofanyika Dar es Salaam.

Kamati iliyoundwa ni Kamati ya Maendeleo ya Miradi ambayo Mwenyekiti wake ni Lucy Mzengi na wajumbe ni Hersi Said, Hamad Ramadhan na Charles Adrian. Kamati ya Rufani za Leseni: Dk Damas Ndumbaro (Mwenyekiti), Dk Alex Mgongolwa (Makamu Mwenyekiti), Charles Matoke, David Kivembele, na Robert Selasela Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji: Elias Mwanjala (Mwenyekiti), Said Soud (Makamu Mwenyekiti), Zakaria Hans Poppe, Issa Batenga, Msanifu Kondo na Said George.

Kamati ya Mashindano: Ahmed Mgoyi (Mwenyekiti), Saloum Chama (Makamu Mwenyekiti), James Mhagama, Patrick Kahemele, Fortunatus Kalewa, Shaffih Dauda, Sarah Chao, Said Tully na Ali Kamwe.

Kamati ya Waamuzi: Soud Abdi (Mwenyekiti), Israel Nkongo (Makamu Mwenyekiti), Zahara Mohamed, John Kanyenye na Samwel Mpenzu. Kamati ya Tiba: Dk Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk Norman Sabuni, Dk Lisobina Kisongo, Dk Eliezer Ndama, Dk Billy Haonga na Dk Violet Lupondo.

Kamati ya Ufundi: Vedastus Lufano (Mwenyekiti), Mrisho Bukuku (Makamu Mwenyekiti), Ibrahim Masoud, Ally Mayay, Michael Bundala, Jumbe Menye na Edibily Lunyamila. Kamati ya Mpira wa Vijana : Khalid Abdallah (Mwenyekiti), Lameck Nyambaya (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Aden, Nassib Mabrouk, Salim Kibwana, Vicent Majili, Kenneth Pesambili, Nicky Magarinza na Philip Alando.

Kamati ya Futsal na soka la ufukweni ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi na Didas Zimbihile. Kamati ya Leseni za Klabu: Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), Sunday Kayuni, George Mayawa na Tumaini Mringo

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi