loader
Picha

Mgunda hesabu zake kwa Yanga

KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amekiri uzembe ulisababisha kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting 2-1, lakini sasa wanajiandaa kupata ushindi kwenye mchezo utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga dhidi ya Yanga.

Mgunda alitoa kauli hiyo juzi baada ya kikosi chake kupoteza mechi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani na kusema ameiangalia Yanga kwenye michezo iliyopita na kugundua udhaifu wao, hivyo anatarajia kuja na mbinu itakayosaidia kupata ushindi.

“Nimeanza kuwapa wachezaji mbinu mpya zitakazosaidia kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Yanga, mchezo ambao tunaamini utakuwa mgumu kwani kila mmoja anahitaji ushindi kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo” alisema Mgunda.

Alisema amegundua wachezaji wake wanakosa umakini kwenye dakika za mwisho akitolea mfano mchezo dhidi ya Azam FC walioshinda kwa mabao 2-1 wachezaji walionesha hali hiyo na kuwafanya kufungwa bao kama walilofungwa dhidi ya Ruvu Shooting.

Mgunda alisema tatizo hilo anaendelea kulifanyia kazi kuhakikisha halijirudii wakati huo wakiendelea kufanya mazoezi ya kukabiliana na Yanga ambayo ina uchu wa kupata ushindi baada ya kupata sare kwenye michezo mitatu mfululizo.

Coastal kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 23 wakishinda michezo 11, sare tano na kupoteza michezo saba. Yanga inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 40 katika michezo 21 iliyocheza ikishinda michezo 11, sare saba na kufunga michezo mitatu.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi