loader
Picha

Watakiwa kulima pilipili hoho ziuzwe nje

WIZARA ya Biashara na Viwanda imewataka wakulima kulima pilipili hoho na mazao mengine ya viungo ambayo soko lake lipo la uhakika pamoja na bei nzuri yenye tija.

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh alisema hayo akizungumzia maendeleo ya kilimo hicho ambacho kilikuwa maarufu katika miaka ya 1970-1980.

Alisema Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) linatakiwa kushughulikia kilimo hicho pamoja na kununua pilipili hoho na kuuza nje ya nchi. Alisema wizara imetenga Sh milioni 500 kwa ajili ya kuimarisha kilimo hicho ambapo kitashughulikiwa na mabaraza ya vijana.

Alisema vijana wataimarisha kilimo hicho kwa kutayarisha mashamba maeneo yaliyotengwa Panga tupu na Bambi wilaya ya Kati Unguja. ‘’Kilimo cha pilipili hoho kitafanywa na vijana kutoka mabaraza ya vijana na kuuza pilipili hoho hizo Shirika la Taifa la Biashara,”alisema.

Hafidh alisema soko la pilipili hoho la uhakika lipo nchi za Arabuni ambapo mazao hayo hulimwa zaidi maeneo ya ukanda wa ardhi yenye mawe.

Alisema wakati umefika Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhamasisha wananchi kulima kilimo cha mazao ya biashara ya viungo. Utafiti umeonesha mazao yenye soko kubwa ni pilipili hoho, pilipili manga, binzari nyembamba, mdalasini na hiliki.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeshauri ujenzi wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi