loader
Picha

TRA yawapa semina ya kodi wafanyabiashara

MAMLAKA ya Mapato ya Tanzania (TRA) imewapa wafanyabiashara ndogo na huduma za usafi rishaji wilayani Muheza mkoani Tanga, semina ya uelewa wa kulipa kodi serikalini.

Mafunzo hayo yalifanyika juzi wilayani Muheza Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaasha Tumbo. Meneja wa TRA Wilaya ya Muheza, Daudi Njohole alisema mafunzo hayo yanalenga kusikiliza changamoto za wafanyabiashara.

Alisema lengo ni kutaka kujua kero za wafanyabiashara wasafirishaji zifanyiwe kazi na elimu hiyo ni endelevu katika wilaya ya Muheza ili kujua kero za wafanyabiashara wote.

Ofisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi Mkoa wa Tanga, Salimu Bakari alisema elimu kwa mlipa kodi ipo chini kwa wafanyabiashara kwa kuwa hawataki kufika TRA na kwenye semina zinazotolewa na TRA, hutuma wawakilishi.

Alisema wameanza mikakati ya TRA kutembea nchi nzima kuanzia Tanga wakipitia duka hadi duka kutoa elimu wafanyabiashara kuhusu kodi. Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha aliomba wafanyabiashara waliopatiwa elimu ya mlipa kodi wawe mabalozi kwa wenzao Aliwataka kuhudhuria semina zinazotolewa na TRA hususani juu ya masuala ya kulipa kodi.

WATU 324 wamewekwa katika sehemu maalumu ya uangalizi, wakiwemo wauguzi ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Muheza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi