loader
Picha

Walimu wapewa mafunzo Tehama

WALIMU 200 wa shule za sekondari za halmashauri nne wilaya za mkoa wa Morogoro wamepatiwa mafunzo ya ufundishaji masomo kwa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) chini ya uwezeshaji wa Mradi African Digital School Initiative (ADSI).

Mratibu wa mradi huo wa Mkoa wa Morogoro, Ramadhani Matimbwa alisema hayo karibuni wakati wa mafunzo ya mwisho kwa walimu katika kufundishia wanafunzi wa shule za sekondari mkoani humo kwa njia ya Tehama.

Matimbwa alisema mradi huo unaoratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la The Global E-Schools and Communities Initiative (GESCI) lililoanzishwa Marekani makao makuu yake ni Nairobi, Kenya na unatekelezwa Tanzania, Kenya na Ivory Coast. Ulianza mwaka 2017.

Mradi huo unamalizika mwaka huu ukinufaisha shule 20 za sekondari za mkoa wa Pwani na Morogoro ambapo halmashauri nne za mkoa huo, Manispaa ya Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Kilosa na Mvomero walimu wake wamenufaika na mradi huo.

Alisema matumizi ya Tehama yameongezeka shule za sekondari kutokana na taasisi zisizo za kiserikali kuelekeza nguvu zao kusaidia shule kwa walimu na wanafunzi kujifunza somo hilo na zinazonufaika zaidi ni shule zenye ufadhili.

“Shule za kata vijijini zimenufaika na mpango wa umeme vijijini na zinaweza kufaidika na mpango wa ufundishaji kwa Tehama,” alisema.

Alisema ili kuifikisha elimu hiyo kwenye shule nyingi zikiwemo za kata ni vyema serikali ikaweka kifungu maalumu cha fedha ili kugharamia huduma za umeme kuendeleza somo hilo shule za sekondari zenye umeme.

Aliiomba serikali kuweka kifungu maalumu cha fedha kugharamia matumizi ya huduma ya mfumo huo shule za sekondari zenye miundombinu ya umeme zikiwemo za vijijini.

Ofisa Taaluma Mkoa wa Morogoro,Vicent Itambu alisema mradi wa ADSI una mafanikio makubwa kwa kufanikisha kufanyika mtihani wa kidato cha pili kwa somo la Information and Computer Studies (ICS) kwa shule za sekondari, jambo ambalo halikuwepo kabla ya mradi huo.

Alitaja changamoto ya shule za mradi huo ni uhaba wa vitendea kazi kufundishia somo hilo, kompyuta na projekta na kukosa uwezeshaji wa kifedha katika matumizi ya kimtandao.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeshauri ujenzi wa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi