loader
Picha

Mwigulu- Nilicheza na Kagere Umisseta

MBUNGE wa Iramba Magharibi Dk Mwigulu Nchemba amesema timu ya Singida United haina tatizo la fedha na wana usafiri mzuri kuliko wa timu ya Simba SC ya Dar es Salaam.

Dk Nchemba amesema kama wangekuwa na tatizo la fedha jamii ingeshasikia siku moja wamekwama hotelini na kwamba, wachezaji wa timu hiyo hawajawahi kulala njaa au kula mlo mmoja.

Amesema wachezaji wa Singida United wanapata mishahara kama inavyostahili na kwamba wanafanya vibaya kwa sababu walisajili vijana wasio na uzoefu.

“Na wana usafiri bora kuliko hata wa Simba, usafiri bora kuliko hata ule wa Simba sisi tulichokosea tu ni kwamba tulichukua vijana ndio maana nimeshajua kwa nini Simba wanasajili wazee ndio maana na mimi nikaona nimlete Haruna Moshi na Chuji…aah nimeshaona bwana kwa nini jamaa wanaleta veterani, Kagere yule tulicheza nae Umisseta (Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania) wakati ule Waziri wao akiwa Saitoti sisi wa kwetu huku akiwa Kapuya”amesema Nchemba alipozungumza wakati wa kipindi cha michezo cha Sports Arena kinachorushwa na redio ya Wasafi FM.

Mwanasiasa huyo amesema anaamini timu ya Singida United itapambana isishuke daraja.

Amesema hashangazwi na matokeo inayopata timu hiyo kwa kuwa yanatokana na ugumu wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara.

Kwa mujibu wa Dk Nchemba tangu ligi ilipoanza amekuwa akipambana kwa ajili mafanikio ya timu hiyo na si kweli kuwa amejiweka kando kwa sababu ya matokeo mabaya inayopata.

Amesema Singida United inapata matokeo mabaya kwa sababu raundi ya kwanza ilisajili wachezaji wasio na uzoefu wakakuta ligi ngumu.

"Raundi ya pili tumebadilisha kikosi sasa hakijaelewana we utaona kwamba mechi hizi zote walizocheza mchezaji wa zamani anakuwa mmoja ama wawili kwa hiyo timu haijaunganika sasa ndio maana timu huwa zinafanya pre season maana huwa ili timu ijuane sasa sisi timu wanajuana ndani ya mechi ndo maana inakuwa shida"amesema.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi