loader
Picha

Serikali kuajiri madaktari 1,000

RAIS Dk John Magufuli ameiagiza Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kuajiri madaktari 1,000 kati za zaidi ya 2,000 wasio na ajira hivi sasa.

Ametoa agizo hilo leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya afya wakiwemo madaktari.

“Tutaajiri madaktari waliosoma miaka mitano, mambo yakiwa mazuri tutaongeza wengine, tunahitahi wajifunze vifaa vya matibabu vya kitaalamu ambavyo vinaletwa nchini,” amesema.

Rais ameagiza pia kuwepo kwa mgawanyo mzuri katika kuwasambaza madaktari watakaoajiriwa ili wapelekwe hadi vijijini.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inatambua kazi nzuri inayofanywa na madaktari nchini na ameahidi kushughulikia changamoto nyingine zinazokabili sekta ya afya.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi