loader
Picha

NEC yaongeza muda kuandikisha Dar

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza kuongeza siku tatu kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura mkoa wa Dar es Salaam.

Hiyo imekuja mara baada ya NEC kufanya kikao cha kutathimini zoezi hilo ambalo awali lilitakiwa kukamilika leo, Februari 20, 2020, hivyo uandikishaji utaendelea hadi Jumapili Februari 23, mwaka 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Wilson Mahera Charles, katika muda huo ulioongezwa vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni.

NEC imewataka wakazi wa Dar es Salaam, kuutumia muda wa nyongeza vizuri kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza.

WATU 324 wamewekwa katika sehemu maalumu ya uangalizi, wakiwemo wauguzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi