loader
Picha

Posho ya wanafunzi China yasitishwa

SERIKALI ya China imesitisha posho ya kijikimu kwa wanafunzi wa kigeni inaowadhamini walioondoka nchini humo hadi watakaporejea vyuoni.

Wanafunzi wa kigeni wapya waliopata ufadhili mwaka wa masomo 2019/2020 wametakiwa kuwasiliana na vyuo wapate miongozo.

Kwa mujibu wa taarifa ya ubalozi wa Tanzania jijini Beijing, Serikali ya China imeruhusu wanafunzi wa kigeni wanaotaka kuahirisha masomo wafanye hivyo kwa kuwasiliana na vyuo wanaposoma.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kwa wanaodhaminiwa Baraza la Udhamini wa Masomo litaidhinisha kuendelea kwa udhamini kwa sharti kuwa kuahirisha kusizidi mwaka mmoja.

Kwa kuzingatia taarifa hiyo, Serikali ya China imewataka wanafunzi wa kigeni wanaosoma nchini humo wasirudi China hadi watakapopewa taarifa kutoka mamlaka za vyuo wanaposoma kuhusu tarehe ya kufungua chuo.

Wanafunzi hao wamehimizwa kuwasiliana na vyuo ili kufahamu kama kozi zao zinaendeshwa kwa mtandao.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, China imetangaza kuwa Serikali za majimbo zitapanga muda wa kufungua vyuo vikuu kwa kuzingatia tathmini ya hali ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.

Serikali hiyo imeagiza wanafunzi wa kigeni wawasiliane mara kwa mara na vyuo wanaposoma kuhusu suala hilo.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imenunua pikipiki saba zenye thamani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi