loader
Picha

Aprili 1 uamuzi kesi ya Halima Mdee

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imepanga Aprili Mosi, mwaka huu kutoa uamuzi kama Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ana kesi ya kujibu au la katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Alidai baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu wa upande wa mashitaka wameona wafunge ushahidi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliwapa siku 14 upande wa utetezi kuwasilisha maelezo kama mshitakiwa huyo ana kesi ya kujibu au la na pia alitoa siku 14 kwa upande wa mashitaka kujibu hoja hizo.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Mdee ana kesi ya kujibu au la.

Katika kesi hiyo mashahidi watatu wa upande wa mashitaka wametoa ushahidi akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi