loader
Picha

Uvamizi wa mifugo shamba la serikali wasababisha kifo

MTU anayedaiwa kuwa ni mhalifu ameuawa na Polisi akiwa njiani kupelekwa hospitalini baada kujeruhiwa kwa risasi na kutokwa damu nyingi zilizosababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema jana kuwa kifo hicho kimetokea Februari 16, mwaka huu saa 10 jioni katika Shamba la Mifugo na Nyasi la Mabuki lililopo Kata ya Mabuki wilayani Misungwi, ambalo ni mali ya serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo.

Alimtaja mtu huyo aliyefariki kuwa ni John Lugata (30) ambaye ni Mkazi wa Manawa aliyejeruhiwa mkono wake wa kushoto ambapo akiwa na wahalifu wenzake walivamia shamba hilo kwa lengo la kuchukua mifugo yao iliyozuiliwa katika shamba hilo baada ya kuingizwa humo kinyume cha sheria, kanuni na utaratibu wa shamba hilo.

Alisema chanzo cha tukio hilo, wafanyakazi wa shamba hilo wakiwa kwenye kazi zao za kila siku walikamata ng’ombe 176 walioingizwa ndani ya shamba hilo nje ya utaratibu na kuizuia, na baada ya mifugo hiyo kuzuiliwa, kundi la watu (wahalifu) lilijikusanya na kwenda katika shamba hilo kwa nia ovu ya kuchukua kwa nguvu mifugo hiyo iliyokuwa imekamatwa na walinzi/wafanyakazi wa shamba hilo.

Kamanda Muliro aliwataja waliojeruhiwa ni Hangwa Masanja (28) ambaye ni mfanyakazi wa shamba hilo aliyejeruhiwa na wahalifu hao kichwani upande wa shavu na sikio la upande wa kushoto kwa jiwe lililorushwa kwa kombeo, ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, na hali yake sio nzuri.

Alimtaja mwingine aliyejeruhiwa ni mfanyakazi mwingine, Benjamin Musa (32) mkazi wa Manawa aliyejeruhiwa na wahalifu hao kichwani utosini kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na kupigwa miguu yote miwili kwa fimbo na ameshonwa nyuzi sita kichwani, ambao alipatiwa matibabu na kuruhusiwa katika Zahanati ya Misasi.

Pia kwenye tukio hilo, Kamanda Muliro alisema walijeruhiwa askari polisi wawili, Konstebo wa Polisi, Mayani ambaye alijeruhiwa kwa kombeo mkono wake wa kulia na Konstebo wa Polisi Mzee aliyejeruhiwa kwa kombeo katika mkono wake wa kulia ambao wote wawili walitibiwa na kuruhusiwa. Kamanda Muliro alisema ng’ombe wote 176 wamelipiwa faini ambapo kila mfugo unatozwa Sh 100,000 na kukabidhiwa kwa wamiliki.

WATU 324 wamewekwa katika sehemu maalumu ya uangalizi, wakiwemo wauguzi ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi