loader
Picha

Waathirika mafuriko Lindi wahitaji mbegu, chakula

MKOA wa Lindi umesema unahitaji chakula, mbegu pamoja vifaa vya ujenzi kwa walioathirika na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za Januari mwaka huu.

Mafuriko hayo yalisababisha watu 24 kupoteza maisha na wengine 8,000 kukosa makazi huku kuku, mbuzi na ng’ombe wanaokadiriwa 5,000 walipotea na mashamba yaliyaharibiwa.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Majid Myao ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa kampuni ya Equinor Tanzania ambapo walileta msaada wa mabati 405, alisema misaada bado inahitajika kwa sasa kwa walioathirika. Alisema kwamba nyumba 4,966 ziliharibiwa na mafuriko hayo na kwa sasa wanahitajika vyakula, mbegu na vifaa vya ujenzi.

Naye Mratibu wa Maafa kutoka Wilaya ya Kilwa, Kasimu Kambiri alisema viwanja 1,528 vilishapimwa na kugawiwa kwa walioathirika ambao hawana makazi ya kudumu. Alisema vijiji 17, tarafa nne na kata nane ziliathiriwa na maafa hayo ya mafuriko, wilayani humo.

Alisema kwamba halmashauri inajitahidi kwa hali na mali hasa kuwasambazia mbegu lakini bado mahitaji yao ni makubwa kuliko uwezo wa mamlaka hiyo. Naye Ofisa wa Kampuni ya Equinor Tanzania inayoshughulikia gesi na mafuta, Naomi Makota alisema kampuni hiyo iliguswa na tatizo hilo la maafa na kuamua kutumia Sh milioni 10 na kununua mabati kwa walengwa wa maafa hayo.

SERIKALI imeombwa kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya vitakasa mikono ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi