loader
Picha

Biashara yajiandaa kisaikolojia kwa Simba

TIMU ya soka ya Biashara United ya Mara imesema inawaandaa wachezaji wake kisaikolojia kuelekea katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba ili wacheze katika hali itakayowapa manufaa.

Biashara United imeshatua Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu kwa ajili ya kusaka pointi tatu zitakazowapa nafasi ya kupanda juu. Akizungumza na gazeti hili jana Kocha Msaidizi wa Biashara, Madenge Omar alisema wanajiandaa kisaikolijia wakiamini Simba wanaitizama kama ni timu kubwa na wanaheshimu ila uwanjani lazima wapambane kupata matokeo mazuri.

“Hatuna wasiwasi na Simba tunawaelewa vizuri ni timu kubwa, tumewasoma tunajua nguvu yao na udhaifu hivyo sisi tunajipanga na malengo yetu ni kushinda,”alisema.

Alisema wanajua watakuja na mbinu gani dhidi ya wapinzani wao, kwani wamepanga kutumia madhaifu ya Simba katika kupata matokeo ya pointi tatu.

“Tunajua namna tutakavyoweka mipango yetu vizuri kwa ajili ya kupata ushindi. Tutatumia madhaifu yao kuwaadhibu,”alisema.

Kocha huyo aliwatoa hofu mashabiki wa Biashara kuwa wasiwe na shaka kwani wametoka kucheza michezo sita bila kupoteza na kwamba anaamini kasi yao itaendelea kuwa bora.

Biashara United inashika nafasi ya tisa kwa pointi 32 baada ya kucheza michezo 23, kushinda nane, sare nane na kupoteza saba huku ikitarajia kukutana na bingwa mtetezi Simba inayoongoza ligi kwa pointi 59 katika michezo sawa na hiyo.

SERIKALI imeombwa kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya vitakasa mikono ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi