loader
Picha

Azam hatoki salama kwetu-Namungo

KOCHA wa Namungo, Hitimana Thierry amesema anajua ubora wa Azam FC kuelekea katika mchezo dhidi yao ila hawawaogopi zaidi ni kujipanga kupata matokeo kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Namungo itakuwa mwenyeji kwa Azam FC kesho katika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi. Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Thierry alisema uwanja wa nyumbani ni mzuri kupata matokeo na kwamba ni lazima wautumie vizuri kwa mechi yoyote.

“Kama ukishindwa kupata matokeo mazuri katika uwanja wako wa nyumbani, upate wapi tena. Sisi tunajipanga na wachezaji wako salama na tayari kuwakaribisha Azam FC,” alisema. Thierry alisema mchezo unaweza kuwa mgumu kwasababu Azam inataka pointi tatu ili kubaki katika nafasi waliyopo.

Timu hizo zimetofautiana pointi nne, Azam ikiwa katika nafasi ya pili kwa pointi 44 na Namungo katika nafasi ya tatu kwa pointi 40 sawa na Yanga iliyo katika nafasi ya nne. Kocha huyo alisema alitumia nafasi ya kuwasoma wapinzani wake hao katika mchezo uliopita dhidi ya Ndanda waliotoka sare ya bao 1-1.

Timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu wa 2019/20 imekuwa katika kiwango bora tangu kuanza kwa ligi na kunyemelea nafasi nne za juu kimya kimya.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi