loader
Picha

Kanyasu ataka fursa za utalii Ukerewe zichangamkiwe

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka wananchi kuchangamkia fursa za utalii zilizopo katika Kisiwa cha Ukerewe.

Akizungumza juzi wakati alipotembelea Kituo cha Urithi wa Utamaduni cha Mapango ya Handebezya kilichopo katika kisiwa hicho mkoani Mwanza, Kanyasu amesema kisiwa hicho ni Zanzibar ya Tanzania Bara.

Alisema kisiwa hicho kina utajiri wa vivutio vya utalii na hakina tofauti na Zanzibar kutokana upekee wake, hivyo amesema kama nchi bado haijakitumia kisiwa hicho ipasavyo kama ilivyo Zanzibar.

Kutokana na kauli hiyo, Kanyasu ameitaka jamii kukitumia kisiwa hicho kama ni fursa ya utalii ili wananchi wenyewe waweze kufaidika kupitia sekta ya utalii kama ilivyo Zanzibar Alisema mbali ya kisiwa hicho kuwa na fukwe nyingi ambazo ni nzuri, pia kina tamaduni za kipekee ambao ni moja ya zao la utalii wenye mvuto wa kipekee unaowafanya watalii wengi kutoka nje ya nchi kuja nchini kwa ajili ya kujionea amali hizo.

Mbali ya vivutio hivyo, Kanyasu alisema katika kisiwa hicho kuna jiwe linalocheza pamoja na jumba lenye ghorofa moja ambalo ni la kwanza kujengwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na ya Kati.

Alifafanua kuwa ngoma peke yake inaweza kumsafirisha mtalii kutoka Marekani kufika Ukerewe kwa ajili ya kuiangalia kwa sababu ina kionjo ambacho hakiwezi kukipata mahali popote duniani. Alifafanua kuwa utalii wa kiutamaduni una ladha isiyoisha kwa vile inahusisha viungo vya mwili kucheza ni tofauti kabisa na mwingine atakavyocheza ngoma hiyo hiyo.

Pia kuna wanyamapori kama vile mamba pamoja na viboko ambao hawajulikani na watalii kama wapo. Kanyasu ameitaka halmashauri hiyo kutoka usingizini kwa kuona kisiwa hicho ni fursa kubwa ya mapato ya utalii kama ambavyo Zanzibar na Kisiwa cha Mafia vinavyofaidika kupitia utalii kwa sababu visiwa hivyo vipo sawa na Ukerewe. Kisiwa cha Ukerewe ni kisiwa cha tano duniani kisicho cha baharini na kina zaidi ya ukubwa wa kilomita za mraba 530.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeshauri ujenzi wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi