loader
Picha

Ndugai awapa neno viongozi wa dini

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kupiga vita unyanyapaaji watu wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwani ni kinyume cha mila na desturi za Kitanzania.

Ndugai alisema hayo jana jijini hapa wakati akifungua mkutano wa siku moja wa viongozi wa dini, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi, Dawa vya Kulevya na Kifua Kikuu na wajumbe wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

Spika Ndugai alisema nafasi ya kufanya hivyo kwa viongozi wa dini ipo kwani kumnyanyapaa mtu mwenye Virusi Vya Ukimwi ni sawa na ubaguzi wa rangi na Watanzania wana upendo na mshikamano hivyo hali hiyo haistahili kuwepo.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk Leonard Maboko alisema watu zaidi ya 24,000 hufaa kwa Ukimwi nchini na 72,000 hupata maambukizi mapya na watu 200 hupata maambukizi kila siku.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo alisema watu wote wana thamani mbele ya Mwenyezi Mungu kama vitabu vya dini vinavyoeleza hivyo kumnyanyapaa mtu ni dhambi na ni kumkosea Mwenyezi Mungu.

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (NACOPHA), Deogratius Rutatwa alisema vijana hawapendi kupima Ukimwi na wakipima na kuanza kupata dawa hukatisha dozi na kukimbia

WALIMU 151 wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi