loader
Picha

Wabunge upinzani ‘wapukutika’, mwingine ahamia CCM

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) amejiuzulu kiti chake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Ijumaa, Februari 21, 2020.

Ahmed ametangaza kujiunga na CCM akiwa katika mkutano wa ndani wa chama hicho tawala katika Jimbo la Nanyamba mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally.

Huu ni mwendelezo wa viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani kutangaza kuhamia CCM wakieleza kuwa ni kutaka kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano.

Mapema wiki hii, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alitangaza pia kuhamia chama tawala akieleza sababu kuwa ni kuchoshwa na malumbano yasiyoisha ndani ya chama kikuu cha upinzani.

Aliyekuwa Mbunge wa Ndanda, (Chadema) Cecil Mwambe pia alitangaza kujiuzulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani na kuhamia CCM wiki iliyopita.

WATU 324 wamewekwa katika sehemu maalumu ya uangalizi, wakiwemo wauguzi ...

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

2 Comments

 • avatar
  Bahati Mukama
  22/02/2020

  But muwe mnatupatia habari Leo mfano jumamosi

 • avatar
  Bahati Mukama
  22/02/2020

  But muwe mnatupatia habari Leo mfano jumamosi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi