loader
Picha

Mbunge wa CUF ahamia CCM

MBUNGE wa Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed (CUF) amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally aliyekuwa katika mkutano wa ndani wa CCM katika Jimbo la Nanyamba mkoani Lindi.

Mbunge huyo amefuata nyao za wabunge kadhaa, waliovihama vyama vyao katika vipindi mbalimbali, ambapo hivi karibuni aliyekuwa Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe alihama Chadema na kurejea CCM.

Pia hivi karibuni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji naye alihamia CCM. Mawaziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa tayari walishahama Chadema na kwenda Chama cha Mapinduzi (CCM). Hatua hiyo ya Katani, inafanya idadi ya wabunge waliohama kutoka upinzani na kwenda CCM kufikia 11 wakiwemo watatu kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Wabunge hao mbali na Mwambe ni Mwita Waitara aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Pauline Gekul (Babati), James Millya (Simanjiro), Joseph Mkundi (Ukerewe), Ryoba Marwa (Serengeti), Julius Kalanga (Monduli) na Dk James Molel kutoka Jimbo la Siha.

Huko nyuma Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru aliwahi kunukuliwa katika mahojiano yaliyofanyika na kituo kimoja cha televisheni, kuwa chama hicho kitaendelea kuwapokea viongozi wa vyama vya upinzani, baada ya kuwasilisha barua zao za kutaka kujiunga na chama hicho, suala linaloleta ishara kuwa linaendelea kutekelezeka.

“Tutaendelea kuwapokea vigogo kutoka vyama vya upinzani. Hatuwezi kuwanyima uhuru wa kuhama vyama vyao. Nina barua za wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga CCM. Nawauliza, hamtaki kiinua mgongo? Wanajibu, potelea pote,” alinukuliwa Dk Bashiru katika majohiano hayo.

Alivishauri vyama vya upinzani nchini kuwa hakuna njia ya mkato ya kuishinda CCM katika uchaguzi. Kwamba ni vyema vijifunze kutokana na uchaguzi mkuu wa 2015, ambapo viliunganisha nguvu zao, lakini vikashindwa kuiondoa CCM madarakani.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi