loader
Picha

Waomba siku 14 kupitia maombi ya wadhamini wa Lissu

UPANDE wa mashtaka wa kesi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini, Tundu Lissu umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam iwape siku 14 kwa ajili ya kupitia na kuchambua maombi ya wadhamini wa mshtakiwa huyo.

Wadhamini wa Lissu kwa nyakati tofauti jana, waliieleza mahakama kuwa wamewasilisha maombi mahakamani hapo, kuomba itoe hati ya kukamatwa kwake ili waweze kujitoa udhamini kutokana na mtuhumiwa huyo kutohudhuria katika kesi yake.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alikiri kupokea maombi yakiambatanishwa na hati ya kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kuomba mahakama iwapatie muda wa kutosha waweze kuchambua maombi hayo.

“Mheshimiwa ni kweli tumepokea hati kiapo cha maombi ya wadhamini, tunaomba mahakama itupatie muda wa kutosha ili tuweze kuchambua maombi hayo kwa sababu maombi hayo yana vitu vingi hivyo mheshimiwa tunaomba utupangie tarehe nyingine,” alisema Simon.

Akijibu hoja hiyo, Hakimu Simba aliwapatia upande wa mashtaka muda wa siku 14. Aliwasisitiza watumie siku 10, kuhakiki maombi hayo kabla ya kurejea mahakamani. Katika kesi ya msingi, Hakimu Simba aliwataka wadhamini kueleza alipo mshtakiwa Lissu, kwa kuwa walishakiri kwamba amepona na mahakama ilihitaji kumuona akihudhuria kesi.

Mmoja wa wadhamini hao, Robert Katula alidai kuwa ni kweli alisema mshtakiwa amepona, ila walipojaribu kuwasiliana naye ili aje mahakamani, alidai ana wasiwasi na usalama wa maisha yake, na ndiyo 1132190012 sababu ameomba mahakama ishughulikie maombi yao.

Kabla ya hakimu kupanga tarehe, wakili Simon alidai kuwa mshtakiwa namba mbili katika kesi hiyo, Simon Mkina hakuonekana mahakamani kwa siku mbili bila taarifa. Aliomba mahakama itakaporudi, mshitakiwa aonywe na na wadhamini wake watoe maelezo ni kwa nini mshtakiwa huyo, hakuhudhuria mahakamani.

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Utetezi, Nyaronyo Kicheere alidai kuwa siku ya jana mshtakiwa Mkina alifika, lakini aliumwa ghafla, akalazimika kurudi nyumbani na bado hali yake si nzuri. Hakimu Simba aliendelea kusisitiza wadhamini wa Lissu, kumleta mahakamani hapo, kwani amri za kesi hiyo bado zinaendelea mpaka zitakapotenguliwa baadaye.

Kesi hiyo iliahirishwa mpaka Machi 10, 2020. Katika kesi ya msingi, Lissu na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka matano, ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho ‘Machafuko yaja Zanzibar.’ Katika shtaka la pili, wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13, 2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi. Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo, pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi