loader
Picha

Maxime awakubali wazawa

KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kutothamini uwezo wa wachezaji wa ndani ni moja ya sababu inayosababisha timu nyingi hususani Simba na Yanga kusajili wachezaji wengi wa kigeni.

Maxime aliyasema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili akijigamba kikosi chake kuwa na wachezaji wazawa na wanafanya vizuri kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na kusema wachezaji wazawa wana uwezo mkubwa kikubwa wanatakiwa kuaminiwa kwenye nafasi zao.

“Wachezaji wazawa wanajua lakini timu nyingi zinashindwa kuthamini mchango wa wachezaji wa ndani ndiyo maana wanavuka mipaka kwenda nje ya nchi kutafuta nyota wa bei ghali ambao wanadhani watakuja kuongeza kitu cha tofauti ndani ya kikosi chao,” alisema Maxime.

Alisema ataendelea kuwa miongoni mwa makocha wanaothamini wachezaji wazawa akitolea mfano kikosi chake kina wachezaji wengi ambao wana kiwango bora kama Awesu Awesu lakini anaanzia benchi.

Pia haoni sababu ya timu kuendelea kusajili wachezaji wa kigeni wanaochukuliwa kwa gharama kubwa lakini baadhi wakisajiliwa wanaonesha uwezo wa kawaida wakizidiwa na wazawa.

Aidha Maxime amethibitisha kikosi chake kimewasili mkoani Dodoma tayari kwa mchezo dhidi ya JKT Tanzania unaotarajiwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Jamhuri na kusema watahakikisha wanapata ushindi kusahihisha makosa yaliyosababisha kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba.

Kagera kwa sasa wanashika nafasi ya sita wakiwa na pointi 37 baada ya kushuka uwanjani mara 23 wakishinda mechi 11 sare nne na kupoteza mechi nane .

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi