loader
Picha

Twiga Stars uwanjani leo Tunisia

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake Tanzania ’Twiga Star’, Bakari Shime amewajenga wachezaji wake kisaikolojia kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Tunisia unaotarajiwa kufanyika leo (saa 9:15 alasiri ) katika Uwanja wa Kram ikiwa ni mechi ya mwisho ya michuano ya Kanda ya Afrika Kaskazini (UNAF).

Shime amekuja na somo hilo la kisaikolojia kuwaandaa wachezaji wake kufuatia mechi iliyopita waliyopoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Morocco, ambapo walifanya makosa yaliyosababisha kuwatoa mchezoni na kuwapa nafasi wapinzani wao kupata bao la ushindi.

“Naamini kupitia kuwajenga kisaikolojia baada ya kupoteza mechi iliyopita kwa mabao 3-2 dhidi ya Morocco, itawasaidia kurudi kwenye hali ya kujituma na kusahau matokeo ya mechi iliyopita,” alisema Shime.

Pia, Shime alisema bado wataendelea kutumia mbinu ya kushambulia kwa kasi baada ya kuwasoma kwenye michezo iliyopia wapinzani wao hao wanaoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa na jumla ya pointi nne.

Alisema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kwamba wanacheza na wapinzani waliopo nyumbani hivyo watakuwa na sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao, hilo haliwatishi.

Bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kujulikana leo, ambapo Morocco wanaongoza kwa idadi ya pointi sita watakabiliana na Algeria. Hadi sasa Twiga Star imeshinda michezo mitatu wakishinda michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja unaowafanya kufikisha jumla ya pointi sita na kushika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo. Michuano hiyo iliyoanza February 14 ilishirikisha mataifa matano, Tanzania, Morocco,Mouritius, Algeria na wenyeji Tunisia.

MSAJILI Msaidizi wa Vyama vya Michezo Jiji la Arusha, Benson ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi