loader
Picha

Amani Sudan Kusini iwe ya kudumu

JUMAMOSI iliyopita dunia ilishuhudia Sudan Kusini ikifungua ukurasa mpya wa maridhiano ya kutafuta amani ya kudumu nchini humo.

Katika kutafuta amani ya nchi hiyo iliyopotea kwa muda mrefu kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalioua mamia ya watu na kuharibu mali mbalimbali, pande zinazosigana, zimefikia muafaka.

Pande hizi ni ule unaongozwa na Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na kiongozi wa upinzani, Dk Riek Mechar ambazo zimekubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa mwishoni Februari 22, mwaka huu. Kutokana na makubaliano hayo, Rais Kiir amemteua Dk Machar kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Mjane wa Mwasisi wa Taifa hilo, Rebecca Garang, kuwa Makamu wa Pili wa Rais.

Kwa mujibu wa mkataba wa amani wa Sudan Kusini, Rais wa nchi hiyo atakuwa ni mmoja, lakini atakuwa na makamu watano, huku mawaziri wakiwa 35, wabunge 550 na magavana wakiwa 10.

Katika kutimiza makubaliano hayo, Jumamosi iliyopita, viongozi walioteuliwa kuunda serikali hiyo waliapishwa ambao ni Makamu wa Rais wanne kati ya watano, Dk Machar kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Rebecca Garang kuwa Makamu wa Pili wa Rais, Dk Waniga kuwa Makamu wa Tatu wa Rais na Taban Deng kuwa Makamu wa Nne wa Rais.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Rais Kiir kukubali kupunguzwa kwa idadi ya majimbo kutoka 32 hadi 10 na Machar kuhakikishiwa usalama wake.

Tukiwa sehemu ya wananchi wa Jumuiya ya Afrika Masharini, tunaunga mkono hatua iliyofikiwa katika kutafuta amani ya kudumu nchini humo.

Hatua hiyo imeleta matumaini makubwa kwa wananchi wa taifa hilo na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla, kuwa taifa hilo sasa litakuwa na amani.

Kufikiwa kwa makubaliano hayo yaliyoratibiwa na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwakilishwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ni faida kubwa kwa Jumuiya ya jumuiya, kwani kutawezesha nchi hiyo kujikita katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi yake badala ya vita na kuimarisha amani katika ukanda huo.

Kufikiwa kwa hatua hiyo si ushindi kwa wananchi wa Sudan Kusini tu, bali Afrika Mashariki kwa ujumla, kwani litakuwa ni eneo lenye umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wake.

Rai yetu kwa viongozi wa Sudan Kusini ni kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makubaliano hayo ili nchi hiyo isirudi tena katika vita iliyoua mamia ya watu wasio na hatia wakiwamo watoto, wazee na wanawake na wengine wakibaki na ulemavu wa kudumu.

Viongozi hao wanapaswa kuweka mbele maslahi mapana ya taifa lao na wananchi, badala ya kutazama zaidi maslahi yao binafsi hasa kupata uongozi.

IMERIPOTIWA kuwa baadhi ya hoteli kubwa nchini, zimeanza kusitisha huduma ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi