loader
Picha

Wanafunzi 47 Dodoma wajazwa mimba

WANAFUNZI wa kike 47 katika shule mbalimbali za sekondari katika wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wameachishwa masomo kwa kupata ujauzito kwa kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mpwapwa, Nelson Milanzi wakati akizungumza na gazeti hili ofisi kwake mwishoni mwa wiki.

Milanzi alisema suala la mimba shuleni linawaumiza vichwa viongozi na wazazi kwani linakwamisha watoto wa kike katika kufikia ndoto za maisha yao.

“Tunapozungumzia suala la mimba shuleni ili kulikomesha, tunahitaji ushirikiano wa hali ya juu kuanzia jamii, vyombo vya kutoa uamuzi hadi viongozi wenye dhamana mbalimbali katika serikali.

“Kushuka kwa maadili katika jamii ndicho chanzo kikuu cha wanafunzi kupata mimba katika umri mdogo ambako kunasababishwa na watu wakubwa wanaoshirikiana nao, wakati mwingine wazazi na jamii inaona wanaingia nyumba ya wageni lakini hawachukui hatua wala kutoa taarifa,”alisema.

Uchunguzi uliyofanywa na gazeti hili baada ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi waliopata ujauzito (majina yamehifadhiwa) walisema, kuna baadhi ya viongozi wa dini, vijana wa bodaboda na watumishi wa serikali wamekuwa wakiwarubuni kwa kuwaaahidi vitu vingi zikiwemo zawadi kama simu na nguo.

“Wengi wanaopata mimba huamua kuzitoa ili kupoteza ushahidi, mimi siwezi kata kata kutoa mimba, siwezi kuua kwa kumtunzia siri mtu bora nipambane na hali yangu,” alisema msichana mmoja.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alikaririwa akisema hana uvumilivu kwa mtu yeyote anayejihusisha kimapenzi na mwanafunzi na kwa mujibu wa sheria kifungu na 130 (1) e na 131(1) (2) ya kanuni ya adhabu namba 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 inamtia hatiani mtu yeyote anayefanya mapenzi na mtu mwenye umri chini ya miaka 18 kwa kupewa kifungo cha miaka 30 jela.

“Ukiona mtu anampa mwanafunzi mimba, utambue kuwa huyo mtu alifanya ngono zembe ambayo inamsababisha kujiingiza katika hatari ya kuambukizwa Ukimwi na magonjwa ya zinaa,”amesema.

Shekimweri alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kuhusu gesti bubu ambazo zimekuwa maficho ya wanafunzi kupatia mimba. Pia aliitaka jamii kutoa taarifa za mtu yeyote anayejihusisha kimapenzi na mwanafunzi ili kuchukua hatua za kisheria stahiki.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Mpwapwa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi