loader
Picha

Simba mechi 10 bingwa

MNAHABARI! Baada ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kupigwa mwishoni mwa wiki iliyopita, klabu ya Simba imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kuutetea ubingwa wao ambapo inahitaji kushinda mechi tisa ili watangazwe mabingwa.

Hesabu zimekaa hivi, Simba ambao Jumamosi walipata ushindi wa mabao 3-1 kutoka kwa Biashara United kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, inahitaji pointi 28 tu ambazo watazipata baada ya kushinda mechi 10 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ile.

Mabingwa hao mara mbili mfululizo msimu wa 2017/18 na 2018/19, kwa sasa wana pointi 62 walizozipata katika kwenye mechi 24 walizocheza.

Hesabu zinaonesha kuwa katika mechi 38 za msimu mzima hivyo amebakiwa na mechi 14 ambazo ni sawa na pointi 42 hivyo kama atashinda zote atafikisha jumla ya pointi 104.

Wanaoshika nafasi ya pili ni Azam FC ambao wana pointi 45 walizozipata kwenye mechi 24 walizocheza mpaka sasa, nao wamebakisha mechi 14 kukamilisha msimu, wakishinda zote watafikisha pointi 87.

Nafasi ya tatu inakaliwa na Namungo FC walio na pointi 43 baada ya kushuka uwanjani mara 23 na wao kama watashinda mechi zao 15 zilizobaki watafikisha pointi 88.

Wapinzani wa jadi wa Simba, Klabu ya Yanga ambao Jumapili walitoka suluhu ugenini mbele ya Coastal Union ikiwa ni sare yao ya nne mfululizo, wana pointi 41 walizozipata kwenye mechi 22 walizocheza, wamebakisha mechi 16 hivyo kama watashinda zote watafikisha pointi 89.

Kwa maana hiyo ukichukua pointi 62 walizonazo Simba, jibu litakuwa wanahitaji pointi 30, ambapo jumla zitakuwa 92, si Yanga, Namungo wala Azam, ambayo itaweza kuzifikia.

MSAJILI Msaidizi wa Vyama vya Michezo Jiji la Arusha, Benson ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi