loader
Picha

Naomie Miss Rwanda 2020

NAOMIE Nishimwe ndiye Miss Rwanda 2020 baada ya kuwashinda washiriki wenzake 19 katika fainali iliyofanyika katika ukumbi wa Intare.

Nishimwe, ambaye amemaliza shule hivi karibuni na ni mwakilishi kutoka Jiji la Kigali katika hatua ya awali ya mashindano hayo, alitangazwa kuwa mshindi wa kwanza katika shindano hilo la urembo, akichukua nafasi ya Meghan Nimwiza, ambaye ni Miss Rwanda 2019.

Phiona Umwiza alifanikiwa kushika nafasi ya pili, akifuatiwa na Denise Mutesi, kama mshindi watatu wa shindano hilo, ambalo lilihudhuriwa na watazamaji wengi.

Kwa upande mwingine, Naomie Nishimwe pia ameshinda taji la Miss Photogenic, Phiona Umwiza amekuwa Mrembo aliyependwa zaidi na watu, huku Nicole Ndenga Teta amekuwa Miss Heritage, wakati Alliance Irasubiza amekuwa mrembo maarufu zaidi.

Washindi walichaguliwa na jopo la majaji, ambao ni James Munyaneza, Jolly Mutesi, Sherrie Silver, Evelyne Umererwa, waliongozwa na Diogene Ntarindwa Mshindi huyo ameondoka na gari mpya aina ya Suzuki Swift, na pia atakuwa akipata mshahara wa fedha za Rwanda 800,000 kila mwezi pamoja na bidhaa zingine kutoka washirika wa Miss Rwanda.

Pia mrembo huyo ataiwakilisha nchi katika shindano la Miss World 2020.

Mwalimu wa kimataifa wa miondoko, Sherrie Silver pamoja na Miss Tanzania, Sylivia Sabastian walishuhudia shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Watu hao maarufu walipokewa kwenye Kiwanja cha Ndege na Miss Rwanda aliyekuwa akimaliza muda wake, Niwemwiza Meghan 2019 pamoja na waandaaji wa shindano hilo.

Miss Tanzania Sylivia alialikwa na waandaaji wa Miss Rwanda na ilielezwa kuwa angekuwa mmoja wa majaji wa shindano hilo la mwaka huu.

MSAJILI Msaidizi wa Vyama vya Michezo Jiji la Arusha, Benson ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi